Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi wakwanza kushoto akitoa maelezo juuya haki za binaadamu kwa mujibu wa Uislam wakati alipokuwa akifunguwa Mafunzo ya Haki za Binaadamu na kuwatambulisha wasaidizi wa Sheria kwa Viongozi wa Dini, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Harusi Miraji na mwisho Jina Mwinyi Waziri Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma na Sheria.
Sheikh Thabit Nooman Jongo kutoka Afisi ya Mufti Zanzibar akiwafahamisha jambo washiriki wa mafunzo ya Haki za Binaadamu katika Ukumbi wa Mazsons Hotel mjini Zanzibar
Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar 26/08/2015.
Mashekhe na Walimu wa Madrasa wametakiwa kuwashajihisha Wananchi ili waepuke kujiingiza katika makundi yanayoweza kuvunja amani katika kipindi hiki cha Mchakato wa Uchaguzi Mkuu nchini.
Hayo yameelezwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi alipokuwa akifunguwa mafunzo ya Haki za Binaadamu yaliyoandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na kufanyika katika ukumbi wa Mazsons Hotel,Shangani Mjini Zanzibar.
Mtakapowaachia huru wale mlowapa kesi si Zao ila kwa kusema kwao ukweli ndio tutajua nyinyi Ni watu mnao ongozwa Na hizo haki Na utawala bora mnazosema.vinginevyo Ni filam ya Andhar Kanoon.
ReplyDelete