Mwamoto akionyesha fomu ya ubunge kulia kwake ni dada wa prof Peter
Msolla Anna Msola na kutoka kulia ni msimamizi mkuu wa uchaguzi Rukia Mhango na
Msaidizi wake
Na MatukiodaimaBlog, Kilolo
Mgombea mteule ubunge ccm jimbo la Kilolo Venance Mwamoto ametangaza
msahama kwa wajumbe wa kamati ya siasa na wagombea udiwani ambao walikuwa
upande wa mbunge wa zamani Prof Peter Msolla huku akiwataka kupenda ili
kuwezesha jimbo hilo kupiga hatua ya kimaendeleo
Mwamoto alisema kuwa hana kinyongo na mgombea yeyeto Kati ya wagombea 15
waliojitokeza na kumwomba prof Msola kuonyesha ushirikiano katika kampeni ili
kuwezesha ushindi kwa Mgombea urais wa Ccm Dr John Magufuli ,ubunge na Madiwani
wote wa CCM.
Mwamoto ametoa kauli hiyo Mchana wa leo wakati akitoa kuchukua fomu ya
ubunge na kuwawapongeza wagombea hao wa ccm udiwani kwa kuteuliwa huku
akiahidi kuwapa ushirikiano mkubwa katika kata zao ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha mabango Yake yanakuwa na picha ya diwani kwa kata husika.
Kwani alisema haipendezi kuona makundi ya kampeni z kura za maoni
yanaendelea katika jimbo na kata za jimbo la Kilolo. Hivyo aliwataka wagombea hao wa udiwani kuandika barua za kuwapongeza
kwa kushiriki kura za maoni wale wote waliogombea nao pamoja na kuwaomba
kushiriki kampeni badala ya kuwabagua na kujigamba kwa kushinda.
Alisema jimbo hilo ili lipige hatua katika maendeleo linahitaji umoja
zaidi toka kwa mabalozi, wenyeviti, Madiwani na mbunge
Huku akiwataka Madiwani hao baada ya kushinda kutokwenda katika vikao
vya madiwani bila kufanya mikutano na wananchi.
" Ni marufuku kwa diwani hata Mimi mbunge kwenda bungeni bila ya
kuchukua kero za wananchi kwenda bungeni ama katika mabaraza ya Madiwani bila
kukutana na wananchi si uwakilishi unaotakiwa "
Mwamoto alisema kuwa jimbo hilo la Kilolo anataka liwe jimbo la mfano
kwa maendeleo katika Mkoa wa Iringa hivyo Kazi Yake kubwa kwa sasa ni
kuhakikisha anabainisha changamoto zote na kuanza na chache katika utekelezaji.
Msimamizi mkuu wa uchaguzi jimbo la Kilolo Lukia Mhango alisema kuwa
jumla ya vyama vitatu vimechukua fomu ya ubunge kikiwemo chama cha mapinduzi
,Chausta na ACT wazalendo huku akisema ruksa kwa wagombea kuchukua na kurejesha
fomu kwa shamra shamra.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...