Katika hali isiyokuwa ya kawaida Chama cha Mapinduzi kimeendelea kupoteza wanachama  wake mara baada  Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole pamoja na Katibu Mwenezi wa Mkoa huo Isaac Joseph kutangaza rasmi kukihama chama hicho cha CCM na kujiunga na CHADEMA.

Uamuzi huo ulifanyika jana jijini Arusha katika moja ya hotel maarufu ambapo viongozi hao walipata wasaa wa kupokelewa na uongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo  Ole Nangole  wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchama wa chadema alisema kuwa CCM hivi sasa imekosa misingi iliyounda chama hicho ya haki na usawa na kuongeza kuwa hivi sasa kimekuwa ni chama cha watu wachache ambao wamekuwa wakichukuaa maamuzi kwa faida yao.

“Nasema CCM imekosa misingi iliyounda chama hiki hakuna haki yeyote inayotendeka imekuwa chama cha watu Fulani ambao wamekuwa wakichukua maamuzi ya kukurupuka kwa faida yao”alisema Nangole.

Kwa upande wake  Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha Isaac Joseph Maarufu kama Kadogoo alisema  kuwa kudhirisha kuwa CCM sasa inaendeshwa kwa maslahi ya watu wachache, mchakato wa kumpata mgombea Urais wa CCM uligubikwa na mizengwe na kusema kuwa kama kanuni na taribu zingefuatwa ni Edward Lowasa ndiye angechaguliwa katika mchakato ule.

Pia alisema kuwa hawezi kukaa na kuongoza katika chama ambacho wafuasi wake wamekihama ,huku akidai kuwa kwa Arusha mjini alikuwa na wafuasi elfu ishirini na saba na waliojitokeza kupiga kura ya maoni ya kumpendekeza mgombea ubunge kupitia CCM ni elfu tano.

“ Siwezi kubaki kuongoza katika chama  ambacho kinabaka demokrasia Uongozi wa CCM watafute viongozi wengine wa kuongoza chama hicho siko tayari na siwezi tena”alisema Kadogoo.

Mwenyekit wa CHADEMA Wilaya ya Arusha Magoma Derick Magoma akiwapokea wanachama hao kutoka CCM na kuhamia rasmi CHADEMA anawakaribisha wote wanaoijisika kuunga nao na kuleta mabadiliko ya kweli kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.

“Tunawakaribisha wote wanaotaka kuhamia chadema mlango upo wazi mda wowote na siku yeyote mda wa mabadiliko ni sasa”alisema Magoma
kadogooo11111
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo  Ole Nangole kulia akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kuhamia rasmi chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)kushoto ni Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha Isaac Joseph Maarufu kama Kadogoo.(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. HAYA WACHAGA HONGERA KWA KUZIDI KUUNGANA ,MUNGU AKIPENDA MTACHUKUA NCHI, LAKINI SIO MIAKA YA HIVI SASA KARIBUNI, NENDENI KWANZA MKASOMEE MAMBO YA UKABILA HUKO RWANDA NA BURUNDI KWANZA NDIO MJE KUANZA ZOEZI HILI TANZANIA , LAKINI KAENI MKIJUA MCHAGA HANA NAFASI HIO YA KUONGOZA NCHI HII TANZANIA LABDA NCHI IBARIKIWE NA WAUNGUJA KWANZA

    ReplyDelete
  2. Uroho wa madaraka unawasumbua

    ReplyDelete
  3. Kila la heri wanakaskazini, jiungeni pamoja mchukue nchini lkn historia mmeweka kuwa wakwanza kuleta ukabila na ukanda. Sababu zenu za kutoka ccm hazina mashiko bali ni hali halisi ya ubinafsi wenu na ukabila mlionao. Hamtofanikiwa kamwe na mtabaki na ukabila wenu na mtatafutana wenyewe.

    ReplyDelete
  4. Wachaga wangeiongoza nchi ingelikuwa na maendeleo kuliko nchi zote za bara la Africa nenda uchagani ukaangalie kulivyoendelea, Kilimanjaro ni moja mikoa inayoongoza kwa maendeleo wachaga na wapare oyeee juuuu juuu kabisaaaa

    ReplyDelete
  5. Sasa sijui huo Uchagga hapa umetoka wapi au kila mtu anayetoka huko kaskazini ni Mchagga?
    Naona Wachagga wanawapa shida wapeni nchi muone bongo itakavyo changamka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...