TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesikitishwa na kuhuzunishwa na kifo cha mmoja wa wanasiasa wa kongwe nchini, Mzee Peter Kisumo ambaye alipata kuwa Mzee wa Chama cha TANU, Muasisi na mdhaminiwa Chama cha CCM naaliyeshikilia nafasi nyingi za uongozi ndani ya Serikali na utumishi wa umma ukiwemo uwaziri.

“Nimepokea kwamasikitiko makubwa na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Mzee Peter Kisumo ambaye nimejulishwa aliaga dunia jana, Jumatatu, Agosti 3, 2015, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, 
ambako alikuwa anapatiwa matibabu ya figo,”amesema Rais Kikwete katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya MzeeKisumo. 

Amesema RaisKikwete: “Kwahakika, kama taifa letu limeondokewa na kiongozi wa kupigwa mfano katika utumishi uliotukuka wa umma na Chama chetu cha Mapinduzi, na kabla ya hapo Chama cha TANU,ni MzeePeter Kisumo.

 Alikuwa mzalendo wa kweli. Alikuwa Mtanzania halisi ambaye hakusita kutetea maslahi ya taifa lake. Katika nafasi zote za uongozi wa taifa letu alizozishikilia – Ubunge, UkuuwaMkoa, Uwaziri, Udhaminiwa Chama Chetu – daimaalionyeshauongoziwakiwango cha juu. 

Alikuwa mwadilifu na mwaminifu na wala hakusita kuyasemea kwanguvu zake zote na kuyatetea yale aliyoyaamini na yale yaliyohusu ustawi wanchiyetu.” Ameongeza Rais Kikwete: “Mzee Kisumo ametuacha wakiwa. 

Tumeondokewa na Mzee hodaria mbaye busara zake na ulezi wake vilikuwa bado vinahitajika sana katika taifa letu kwanyakati za sasa. Tutamkumbuka daima.” 

Katika salamu hizo kwa familia, Rais Kikwete amesema: “Nawatumieni salamu za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo cha Mzee wetu.

 Huyu alikuwa Mzee wenu kama alivyokuwa Mzee wangu na Mzee wa taifa letu na hivyo msiba huu ni wakwetu sote. 

Naungana nanyi katika majonzi na maombolezo. Kwapa moja tuna mwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, atupe subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

 Aidha, tunamwomba Mungu aiwe kapeponi roho ya Marehemu Mzee Peter Kisumo. Amen” 

Imetolewana: KurugenziyaMawasilianoyaRais, Ikulu,
 DAR ES SALAAM. 4 Agosti, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...