Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi zinazojengwa na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu pamoja na Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu
akizungumza jambo na Rais Dkt Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe
la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30za makazi zinazojengwa na
NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,Kulia
ni Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John
Pombe Magufuli wakiondoka eneo la tukio mapema leo mchana.
Sehemu kivuko hicho kilichozinduliwa Rais Dkt Jakaya Kikwete mapema leo mkoani Mtwara.
Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt Jonh Pombe Magufuli akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini baada ya uzinduzi wa kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3,Dkt Magufuli amesema kuwa Rais Jakaya Kikwete katika utawala wake ndani ya maiaka kumi amefanikiwa kujenga vivuko vipya 15 na vingine 7 vimekwishakarabatiwa na vinafanya kazi mpaka sasa
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini kuzindua kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
Bango la mradi huo
Mkuruegenzi Mkuu wa NHC,Nehemia Mchechu akizungumza jambo mbele ya mgeni rasmi Rais Dkt Jakaya Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi kwa ujumla katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi zinazojengwa na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa Msanga
Mkuu-Mtwara vijijini waliofika kwenye uzinduzi wa kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa
kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi
bilioni 3.3
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...