Rais Mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings akisikiliza kwa makini taarifa fupi iliyosomwa mbele yake na Afisa mkuu wa ubalozi wa Ghana hapa Tanzania Dr. Ken Kwaku kuhusiana na utendaji kazi wa Ecobank nchini Ghana na bara la Afrika kwa ujumla na kuzungumzia mikakati ya kudumisha uhusiano na kupanua wigo wa kibiashara kati ya Ghana na Tanzania. (Katikati) ni Balozi wa Ghana nchini Kenya Mhe. Karim. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
(Wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi mkuu wa Ecobank nchini Tanzania Mr. Enoch Osei-Safo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, wateja wa Ecobank na wageni waalikwa wakimsikiliza kwa makini Rais mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings aliyekua akiongea kuhusiana na mikakati ya kupanua wigo wa biashara kati ya Ghana na Tanzania kupitia benki hiyo. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
Rais Mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings akizungumza wakati wa mkutano uliowakutanisha wafanyakazi wa Ecobank Tanzania, raia wa Ghana wanaoishi nchini Tanzania, wateja wa Ecobank na wageni waalikwa jijini Dar es salaam kuzungumzia mikakati ya kudumisha uhusiano na kupanua wigo wa biashara kati ya Ghana na Tanzania. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya kimataifa ya Serena, Dar es salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...