Mkufunzi na Mwandishi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Zanzibar Salim Said Salim akitoa mada katika mafunzo ya siku tano juu ya kuandika Habari za Uchaguzi Mkuu yaliyoandaliwa na Shirika la Habari la Marekani Internews kwa waandishi wa Habari wa Zanzibar katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye Ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Mhadhiri wa Sheria, Kitivo cha Sheria Zanzibar University, Ali Uki akionyesha kitabu cha Sheria cha Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na kitabu cha Sheria cha Tanzania na cha Zanzibar ambavyo vinawapasa waandishi wa habari kuvisoma na kuzitumia sheria hizo katika kuandika habari za Uchaguzi Mkuu kwa usahihi.
Mhadhiri wa Sheria, Kitivo cha Sheria Zanzibar University, Ali Uki akisisitiza kitu kwa waandishi wa Habari katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Internews katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...