Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka mtandao wa matapeli wanaojipatia
fedha kutoka kwa wananchi kwa udanganyifu kwamba watawapatia ajira ndani ya Jeshi
la Polisi hasa katika kipindi hiki ambacho Jeshi la Polisi lipo katika mchakato
wa ajira.
Kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa
makini na mtandao wa matapeli hao na kwamba, mfumo wa ajira ndani ya Jeshi la
Polisi ni wa wazi na unafuata taratibu na kanuni za Jeshi la Polisi, hivyo,
Vijana wote waliochaguliwa kujiunga na Jeshi hilo wafuate maelekezo yaliyoainishwa
katika matangazo ya ajira yaliyotolewa kupitia vyombo vya habari pamoja na
tovuti ya Polisi ya www.policeforce.go.tz
ili kuepuka usumbufu na utapeli wa wahalifu hao.
Tunawakumbusha vijana wote
waliochaguliwa kuripoti kwa makamanda wa polisi wa mikoa kabla hawajaripoti
shule ya Polisi Moshi. Hivyo, yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa kamanda wa
mkoa anakotoka hatapokelewa chuoni.
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa wote wenye tabia hiyo ya
utapeli kuacha mara moja na endapo mtu yeyote atabainika hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi yake.
Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi wote wenye taarifa za matapeli hao
kuzifikisha haraka katika kituo chochote cha Polisi kilicho karibu ili sheria
iweze kuchukua mkondo wake.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
hahahahaha ivi mtu unatoa hela kwa ajiri ya kujiunga na polisi hahahahaha kweli bongo pagumu!!wacha niendelee na boksi zangu mpaka giza......
ReplyDeleteAnonymous wa kwanza acha kejeli ndugu, shibe yako, si shibe ya kila mtu. Wewe umeamua kubeba mabox mwenzio anataka kuwa ngunguri, hapo hakuna matata kabisa
ReplyDelete