![]() |
..Meneja masoko na mauzo wa
Kampuni ya Mega Trade Edmundi Rutaraka, akimkabidhi hundi ya Ts
1.5 Milioni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na
burudani mkoa wa Arusha,Mussa Juma kwa ajili ya tamasha la 10
waandishi wa habari mkoa wa Arusha, Manyara na Dar es salam na wadau
wa habari ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa sheikh Amri Abeid,
hafla hiyo ilifanyika jana, Palace Hoteli Jijini. habari na libeneke la kaskazini blog Tamasha la 10 la vyombo vya habari na wadau wa habari mkoa wa Arusha, linatarajiwa kufanyika Agosti 29 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa kushirikisha timu nane ikiwepo timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam. |
Akizungumza na waandishi wa habari, Palace Hotel , Katibu wa
chama cha waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha(TASWA-Arusha),
Mussa Juma, alisema tayari maandalizi muhimu
yamekamilika.
Juma
alisema Tamasha hilo linaloandaliwa na TASWA na kampuni ya Arusha
Media.mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Bia nchini( TBL) kwa miaka 10 sasa,
litashirikisha michezo ya Soka, Mpira wa pete, kuvuta kamba na
kukimbiza kuku.
"tunapenda kutangaza rasmi tamasha la 10 ya TASWA Arusha
litafanyika Agosti 29 na kauli mbiu yetu ni Uchaguzi Mkuu bila vurugu
inawezekana"alisema
Alisema
katika Tamasha hilo, ambalo litashirikisha pia timu za wafanyakazi wa
kampuni ya bia nchini(TBL) Taasisi na Faidika na kampuni ya Pepsi
litaandamana na ziara ya wanahabari kutembelea Hifadhi ya Taifa ya
Arusha.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...