Kutokana na uhaba wa fedha, Busara Promotions inasikitika kutangaza kuwa tamasha la Sauti za Busara mwaka 2016 halitakuwepo, hii itakuwa ni mara ya kwanza ndani ya miaka kumi na tatu Zanzibar kulikosa Tamasha la kimataifa la Sauti za Busara lifanyikalo kila wiki ya pili ya mwezi Februari.

Yusuf Mahmoud, Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Promotions, amesema leo "Uamuzi huu haukuchukuliwa kwa wepesi”. Kawaida huwa tunatangaza tarehe za tamasha mwaka mmoja kabla. Lakini baada ya kufanya tamasha lililopita kwa mafanikio, tumekuwa katika hali ya ukosefu wa fedha kwa toleo lijalo la 2016. 
 
Tulijiwekea  malengo ya kukusanya dola za kimarekani  200,000 kabla ya Julai, wakati tulipokuwa na matumaini ya kutangaza tarehe za Sauti za Busara 2016. Baada ya mikutano mingi na wadau, tulisogeza muda wetu wa kutafuta fedha hadi usiku wa Agosti 19. Kiasi ambacho tuna uhakika wa kukipata kuandaa tamasha lijayo kwa sasa kinasimamia kwenye dola za kimarekani 42,000, hivyo basi bado tuna safari ndefu mbele yetu.
 
Kawaida wakati kama huu, tunakuwa tumeshafika mbali kwenye makubaliano ya mikataba mbalimbali kama ya kukodi ukumbi, ukodishaji wa vifaa, wasanii na mameneja, tunaanza kupanga ratiba, maandalizi ya usafiri na malazi kwa wasanii mapema iwezekanavyo. Shinikizo zaidi, tumekuwa tukipokea maswali kutoka kwa watu mbalimbali duniani kote wakitaka kujua tarehe za tamasha ili waweze kufanya mipango yao ya safari. Mauzo ya tiketi za Sauti za Busara haijawahi kuwa tatizo, lakini hii inasaidia kulipa 30% ya gharama za tamasha ".

Yusuf ameendelea , "Matamasha yanahamasisha vijana kupenda utamaduni wao, hutoa fursa kwa wasanii na wataalamu wa muziki kukutana na kujifunza , yanashawishi uhai wa tamaduni, pia yanatoa nafasi za ajira kwa watu wa ndani na kutoa mifano ya utalii ambayo inathamini na kuheshimu utamaduni wa ndani. Hata hivyo, tangu mwaka  2004 hatuna msaada wowote wa kifedha kutoka serikali ya  Zanzibar, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pamoja na jitihada nyingi, msaada kutoka kwa wahisani, balozi na wafanyabiashara unazidi kupungua siku hadi siku. Busara Promotions ni shirika lisilo la kiserikali; tamasha haliko kibiashara. 
 
Wengine walipendekeza tujaribu kuomba pesa kupitia mitandao. Hata hivyo, kwa kweli ili kuwa endelevu zaidi, kipaumbele chetu kabla ya toleo la 2017  kitakuwa ni kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu na wadhamini na wafadhili ambao wanakubaliana na  mtazamo wetu. Mtu yeyote anaesoma ujumbe huu na ana nia ya kusaidia kuiweka Sauti za Busara hai, kukuza ajira nchini, wakati tunaendelea kuung’arisha muziki wetu wenye utajiri wa mila na kukuza utalii wa kiutamaduni Zanzibar na Tanzania, tafadhali awasiliana nami kupitia Busara Promotions."

Katika kipindi cha miaka kumi na mbili iliyopita, Busara imewavutia maelfu ya wageni kutoka kila pembe ya dunia  kuja Zanzibar , wakati ambayo hakuwa msimu wa wageni wengi . Ndege zote zinazokuja Zanzibar kipindi cha tamasha zinajaa, hoteli na migahawa vinajaa, maduka yaliyopo maeneo ya Mji Mkongwe yanapata wateja wengi zaidi. 
 
Hata makadirio yanaonyesha tangu mwaka 2004 tamasha limekiingizia kisiwa mapato ya kiasi dola za kimarekami milioni 70. Wakati huo huo, Shirika la utangazaji la BBC limeiweka Sauti za Busara kama moja ya "matamasha ya muziki bora na ya kuheshimika  zaidi Afrika ". Pia limeingizwa kwenye CNN "matamasha 7 ya muziki ya kiAfrika unayotakiwa kuyaona" na kileleni kwenye orodha ya AfroTourism ya "Matamasha bora ya Muziki  ”

Yusuf Mahmoud hatimaye alisema " Wakati mwingine ni muhimu kupiga hatua moja nyuma, kabla ya kusonga mbele. Bodi na uongozi wa Busara itafanya kazi kwa bidii zaidi miezi ijayo, ili kuhakikisha  kuanzia mwaka 2017 tamasha linarudi kuwa na nguvu zaid
i. Inawezekana itamaanisha kuhama  eneo, au kulifanya kila baada ya miaka miwili . Hakika vipaumbele vyetu vitakuwa kulifanya tamasha litoe nafasi zaidi kwa  wananchi  , wakati tunaelendea kuomba  kujenga ushirikiano wa muda mrefu , na sekta za umma na binafsi".

Wakati tamasha likiwa kwenye mapumziko, Busara Promotions itaendelea na shughuli zake za kawaida za kukuza muziki wa kiAfrika, kuimarisha uelewa wa watu na kuboresha sekta ya muziki. Kwa mwaka mzima, Busara itahakikisha wasanii wa Afrika Mashariki wanapata mialiko kwenye matamasha mengine ya  kimataifa na kuwezesha kujenga ujuzi kwa wasanii wa ndani na wafanyakazi wa tamasha, kwa njia ya kubadilishana na mafunzo ya uongozi wa  sanaa, masoko, habari na ujuzi wa kiufundi . Kazi hii , ambayo inadhaniniwa na Ubalozi wa Norway , Dar es Salaam , haitotetereshwa  na uamuzi wa kufuta Sauti za Busara 2016 .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...