Ndugu Augustino Ngonyani, anasikitika kutangaza kifo cha Baba yake mzazi Mzee Joachim A. Ngonyani kilichotokea alfajiri ya tarehe 6.8.2015, Dar Es Salaam.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Sinza Makaburini.
Mwili wa marehemu utaagwa tarehe 8.8.2015 Jumamosi saa 3 asubuhi katika kanisa la Mt.. Petro Oysterbay na baada ya hapo kusafirishwa siku hiyo hiyo kwenda Songea kwa Mazishi.
Mazishi ya Mzee Ngonyani yanatarajia kufanyika siku ya Jumatatu 10.08.2015, Kijijini Kwake Parangu, Songea.
Bwana alitoa, Bwana Ametwaa na Jina lake lihimidiwe.
Amen
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...