WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL), Arusha juzi wameungana na familia zao katika tamasha la familia( Family Day),zilizofanyika katika viwanja vya TGT, vilivyopo eneo la Kisongo,nje kidogo ya Arusha.

Aidha katika tamasha hilo wafanyakazi hao na familia zao walipata fursa ya kushiriki michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu,kuvuta kamba,mpira wa mezani,kucheza muziki pamoja na michezo mbalimbali ya watoto.

Kwa mujibu wa Mratibu wa tamasha hilo Optaty Minja,alisema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuonyesha jinsi kampuni hiyo ya bia inavyothamini familia za wafanyakazi wake.

Minja ambaye pia ni Mhasibu wa TBL katika upande wa mashamba,alisema kuwa kuwakutanisha wafanyakazi hao na familia zao kunawasaidia kuweza kufahamiana , na kusaidia kujenga mahusiano mazuri baina ya familia zao,kwani mara nyingi hukutana wakiwa kazini lakini watoto, wake na waume zao hawafahamiani hivyo kupitia siku ya familia husaidia kujenga uhusiano na kufanya kuwa familia moja.

“Kama kampuni tumeona ni jambo zuri familia zetu kukutana leo ili kuonyesha jinsi gani kampuni inathamini familia za wafanyakazi wake ambapo pia tunazidi kufahamiana,kujenga mahusiano mazuri kati yetu na familia zetu kwa ujumla”alisema Minja
Baadhi ya familia za wafanyakazi wa TBL Arusha, wakipata chakula cha mchana katika viwanja vya TGT,vilivyopo eneo la Kisongo,nje kidogo ya Jiji la Arusha,juzi katika sherehe ya familia (family day) ya kampuni hiyo.
Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya TBL mkoa wa Arusha, wakipewa zawadi baada ya kushinda katika michezo mbalimbali iliyofanyika katika sherehe ya familia (family day) ya wafanyakazi wa kampuni hiyo,juzi,jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...