Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB), Luis Benedicto (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo, kuhusu wasiona kutengwa katika mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia hatua ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho, Jonas Lubago na Katibu Mkuu wa (TLB), Emmanuel Simon.
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano  na Chama cha Wasioona Tanzania (TLB) katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii
CHAMA cha Wasioona Tanzania (TLB)   kimesema kuwa hakitawapa kura wanasiasa ambao hawajaweka mazingira wezeshi na  rafiki  kutokana na kutoweka ilani katika  vyama vyao juu ya maslahi  na haki za watu wasioona  nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya Habari Maelezo,Mwenyekiti wa TLB,Luis Benedicto amesema wana mashaka kwa vyama vya siasa nchini kama vitakuwa vimeweka ilani zao sera au kanunizinazoelekeza utekelezwaji wa maslahi ya yanayowagusa moja kwa moja na changamoto za kimaendeleo zinazowakabili watu wasioona.

Benedicto amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Vyama vya siasa havijawashirikisha katika mkutano wowote  juu ya wao kushiriki katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni  mwa Oktoba.
Amesema NEC haijainisha idadi ya watu wasioona waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na wagombea katika nafasi mbalimbali wanaotoka jamii hiyo.
Hata hivyo wanataka vyama vya siasa vina mipango gani kwa siku za usoni katika kushiriki katika majukwaa ya siasa.

Mwenyekiti wa amesema elimu ya uraia vifaa vya kupigia kura na miundombinu wezeshi juu ya kuweza kufikia vituo vya kupigia kura ni kitendawili ambavyo mpaka sasa bado havijpatiwa majibu na kufanya jamii hiyo kuwa njia panda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...