Rais wa VICOBA Endelevu, Devota Likokola, (Watatu kushoto), akinyanyua juu, mfano wa ATM kadi ya Benki ya Posta Tanzania, TPB, wakati wa uzinduzi wa kadi hiyo itakayotumiwa na wanachama wa VICOBA Endelevu kota nchini. Uzinduzi huo ulifanyika leo Agosti 15, 2015 kwenye bustani ya kumbukumbu ya mashujaa, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Moses Manyanta, Mwenyekiti wa Bodi wa Wadhamini ya Benki hiyo, Profesa Lettic Rutashobya, na Katimu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezweshaji Wananchi Kiuchumi, NEEC, Beng’ Issa.(Picha na Habari na K-VIS MEDIA)

BENKI ya Posta Tanzania, TPB, imezindua rasmi kadi maalum ya ATM kwa ajili ya wanachama wa kikundi cha, VICOBA Endelevu.
Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika kwenye bustani ya kumbukumbu ya Mashujaa, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2015, ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TPB, Profesa Lettic Rutashobya, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEEC), Beng’ Issa, walishuhudia Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Moses Manyanta, akimkabidhi mfano wa kadi hiyo ya ATM, Rais wa Vicoba Endelevu, Devota Likokola mbele ya mamia ya wanachama wa Vicoba Endelevu kutoka sehemu mbalimbali nchini.
Benki ya Posta Tanzania, imeingia mkataba na Vicoba Endelevu, wa kuwapatia mikopo midogomidogo wananchama hao chini ya udhamini wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, NEEC, ili kukuza mitaji na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.

 Wana VICOBA Endelevu wakiingia kwenye bustani hiyo kwa maandamano. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...