Tuzo za makampuni 100 ya kiwango cha kati nchini kutolewa hapo kesho katika hafla itakayofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City. Hayo yamebainishwa hii leo katika mkutano uliowakutanisha wadau wote walioshiriki katika mchakato huo pamoja na waandaaji na wadhamini uliofanyika hii leo katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam. Mchakato huu uliratibiwa na KPMG na Mwananchi Communications Ltd na kudhaminiwa na Benki M.
Mkurugenzi Mkuu wa KPMG Bw. David Gachewa akizungumza katika mkutano huo, KPMG na Mwananchi Communications Ltd ndio waratibu wa mchakato huo chini ya udhamini wa Benki M.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la biashara la Africa Mashariki (EABC) Bw. Felix Mosha akizungumza na wadau wa tuzo za makampuni 100 ya kiwango cha kati nchini katika mkutano wa wadau uliofanyika leo hii katika hoteli ya Hyatt Regency.Hafla ya ugawaji tuzo hizo itafanyika hapo kesho kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Waandaaji wa mchakato wa tuzo za makampuni 100 ya kiwango cha kati nchini wakifuatilia mkutano wa wadau wa tuzo hizo hii leo katika hoteli ya Hyatt Regency, kutoka kushoto ni Mhariri Mkuu wa Mwananchi Communications Ltd Bwn.Bakari Machumu, Mkurugenzi Mkuu wa Research Solutions Africa Bwn. Jasper Grosskurth,Mkurugenzi wa KPMG Bwn. David Gachewa na Naibu Mkurugenzi mkuu wa Benki M Bi. Jacqueline Woiso.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...