Baada ya kukamilika kwa zoezi la Uboreshaji Tume imekuwa ikichakata (processing) taarifa za Wapiga Kura ili kuweza kuandaa Daftari la Awali la Wapiga Kura, katika maandalizi hayo mifumo imeweza kugundua kasoro mbali mbali ambazo baadhi zimefanyiwa kazi na zingine zinaendelea kufanyiwa kazi, kasoro hizo ni pamoja na Wapiga Kura Kujiandikisha zaidi ya mara moja.
Mfumo wa BVR unao mfumo mdogo wa “Mini AFIS” unaoweza kubaini Mpiga Kura anayataka kujiandikisha zaidi ya mara moja katika kituo husika, mfumo huo ulikuwa umeandaliwa ili kuweza kubaini Wapiga Kura wanaotaka kujiandikisha zaidi ya mara moja na kuzuia Uandikishaji huo katika BVR Kit yoyote. Hii ingewekana iwapo Mfumo wa mawasiliano ungekuwa na nguvu katika vituo vyote na kuweza kuwasiliana na mifumo iliyoko katika kituo kikuu cha maandalizi ya Daftari(Data Processing Center) kwani katika kituo hicho imewekwa mifumo ya hali ya juu inayoongoza kimataifa katika kulinganisha alama za vidole na kubaini waliojiandikisha zaidi ya mara moja.
Kwa kutokuwa na mawasiliano yenye nguvu kutoka katika kila kituo Tume ilianza kulinganisha taarifa za Wapiga Kura mara tu baada ya taarifa kufikishwa katika kituo cha maandalizi ya Daftari hivyo kwa mitambo iliyopo Tume imebaini Wapiga Kura wote waliojiandikisha Zaidi ya mara moja ambao taarifa zao zimeisha chakatwa ambao kwa sasa imefikia 52,062 Idadi hii inaweza kuongezeka au kupungua kulingana na uchakataji wa taarifa.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...