SIKILIZA kionjo cha hotuba ya Kiswahili ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez hapa chini.

Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge (wa pili kushoto) akiwasili kwenye kijiji cha Marua kata Kiruavunjo, mkoani Kilimanjaro kwa ajili kupanda miti ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa na kupokelewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto).(Pichazote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
*Sehemu ya Shamra shamra za maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa
Na Mwandishi wetu, Moshi
MASHIRIKA ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini yameadhimisha miaka 70 ya kuundwa kwa umoja huo kwa kupanda zaidi ya 2000 katika miteremko ya mlima Kilimanjaro.
Kazi ya kupanda miti ilifanywa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wadau wao ikiwemo serikali ya Tanzania pamoja na wanakijiji.
Kazi ya kupanda miti iliongozwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishirikiana na Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge.
Shughuli hizo za kupanda miti zilifanyika katika kijiji cha Maruwa.
Akizungumza wakati wa shughuli hiyo Waziri Mahenge alisema kwamba amefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na Umoja wa Mataifa ya kuadhimisha miaka 70 kwa kuwakumbusha washirika wao wa maendeleo suala la mazingira.
“Ni kawaida kuadhimisha kuundwa kwa Umoja wa Mataifa Oktoba 24 kila mwaka. Mwaka huu ni tofauti na zaidi ya tofauti umekuwa maalumu kwa namna yake kwa kuwa tunaadhimisha miaka 70 ya uwapo wa Umoja wa Mataifa.” alisema Waziri Mahenge.

Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi Fionnuala Gilsenan akiwasili kwenye sherehe ya kupanda miti katika kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa na kusalimiana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem.
Hata hivyo alikumbusha kwamba wakati tunaadhimisha miaka 70 ni vyema wadau wa maendeleo wakaangalia historia na kujipanga kimkakati katika kusonga mbele kimaendeleo kwa kujali mazingira.
Alisema kwamba pamoja na hoja ya kujali mazingira pia serikali itaendelea kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mambo mbalimbali ya maendeleo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...