Mgeni rasmi, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Dkt. Ahmed Makuwani kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii akiwahutubia Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akielezea umuhimu wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa maelezo ya awali wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mgeni rasmi, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Dkt. Ahmed Makuwani kutoka Wizara ya Afya na Usitawi wa Jamii (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria Tanzania wa mwaka 2015 mara baada ya kufunga mafunzo ya utafiti huo wilayani Moshi, Kilimanjaro. 

(PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

NA VERONICA KAZIMOTO.
Wito umetolewa kwa viongozi wote wa Serikali katika Ngazi zote na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa Wasimamizi, Wahariri na Wadadisi wa Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria utakaoanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2015.

 Wito huo uletolewa leo na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Ahmed Makuwani wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika wilayani Moshi, Kilimanjaro.

"Ninawaomba Wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Wadadisi, Wasimamizi na Wahariri watakaoshiriki zoezi la kukusanya Takwimu za Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 ili kupata taarifa muhimu na sahihi kwa ajili ya kupanga Mipango na Sera endelevu za Sekta ya Afya katika nchi yetu, amesema Makuwani".

Dkt. Makuwani amesema kuwa taarifa zitakazokusanywa kwa wananchi kwa ajili ya  utafiti huo zitakuwa ni siri na zitatumika kwa shughuli za Kitakwimu tu na wala hazina uhusiano wowote na Uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.

kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema utafiti huu wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015  unalenga kukusanya taarifa nyingi za sekta ya afya zinazotumika katika kutathmini malengo mbalimbali na pia kusaidia katika kupanga mikakati mipya.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mara nyingine tena inafanya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Malaria wa mwaka 2015 ambao kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2010. Utafiti huu utaanza rasmi tarehe 21 Agosti, 2015 kwa nchi nzima na utamalizika mwishoni mwa Mwezi Februari 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...