Na Hillary Shoo, SINGIDA.
MKUTANO Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Singida umemchagua, Fancy Nkuhi kuwa Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Viti maalum kupitia vijana.
Katika uchaguzi uliofanyika jana kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Singida Fancy mwenye Shahada ya pili ya mahusiano ya Kimataifa alipata jumla ya kura 21 huku mpinzani wake Jamila Kitila akiambulia kura 8.
Kwa mujibu wa Katibu wa UVCCM, Mkoa wa Singida Ramadhan Kapeto alisema umoja huo una jumla ya wajumbe 45 lakini waliohidhuria mkutano huo ni wajumbe 29 tu.
Hata hivyo Fancy atawakilisha Mkoa huo kwenye kinyang’anyiro cha kuomba kuteuliwa kuwa Mbunge kupitia umoja huo na kupambana na wagombea kutoka mikoa mingine.
Kapeto alisema nafasi 10 zimegawanywa kwa Zanzibar kuwa na nafasi nne na Bara nafasi sita za kuwakilisha Ubunge kupitia umoja huo.
Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo alikuwa Kaimu Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Singida Mary Maziku akisaidiwa na mchumi wa CCM Mkoa huo Ahmed Kaburu.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoa wa singida kabla ya uchaguzi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...