Mwenyekiti na mwanzilishi wa kikundi cha vijana cha Tanzania Youth Network (TYN), Agnes Mgongo akizungumza na vijana mara baada ya kukutana katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam leo.
Afisa vijana wa wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo, Racheal Kasanda akizungumza na vijana mbalimbali waliounda kikundi kiitwacho Tanzania Youth Network (TYN), wakijadili changamoto mbalimbali zinazowakumba vijana pamoja na vijana kuunda vikundi mbalimbali ili kutumia fursa zilizopo hapa nchini na Nje ya nchi ameyasema hayo katika mkutano uliowakutanisha vijana hao katika ukumbi wa Don bosco jijini Dar es Salaam leo.
Afisa vijana wa wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo, Racheal Kasanda akipokea kitabu cha ujasiliamali kutoka kwa Balozi wa vijana wa jumuia ya Afrika Mashariki, Eric Ngilangwa katika mkutano wa vijana uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa vijana wa wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo, Racheal Kasanda akiwa katika picha ya pamoja na kikundi kilichowakusanya vijana mbalimbali kutoka Bagamoyo,Morogoro pamoja na Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii. Picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...