Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania Limited leo imemtangaza Mkurugenzi wake mpya Bw. Ian Ferrao anayechukua nafasi ya Mkurugenzi anayeondoka Rene Meza ambaye hivi karibinu aliteuliwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Ooredoo Myanmar kuanzia mapema mwezi ujao. 
Bw. Ferrao kwa sasa hivi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Lesotho.Ana uzoefu mkubwa wa uongozi katika sekta ya mawasiliano katika nchi mbalimbali za Ulaya na Afrika.Kabla ya kjiunga na Vodacom Lesotho alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu anayesimamia biashara za kampuni ya Vodacom barani Afrika na alikuwa na hisa katika kampuni ya Africonnect ya nchini Zambia.
Ujio wake kuongoza Vodacom Tanzania ni kama vile amerejea nyumbani kwa kuwa wazazi wake waliwahi kuishi nchini tangu mwaka 1952 kabla ya kuhamia nchini Uingereza mwaka 1970. 
Akiongelea uteuzi wake alisema “mimi ni mzoefu na nina ujuzi wa kuongoza sekta ya mawasiliano na nina imani sekta hii ni zaidi ya mwasiliano bali imeonyesha mabadiliko makubwa katika kuchangia kuleta mabadiliko kwenye jamii kwa kuboresha maisha ya watu na kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri ya kuishi.
Nina imano Vodacom ina uwezo wa kuendelea kuboresha mawasiliano nchini na kuzidi kufanya maisha ya watanzania kuwa murua” 
Naye Rene Meza Mkurugenzi aliyeiongoza Vodacom Kuanzia mwaka 2011 alisema kuwa katika kipindi cha uongozi wake Vodacom Imefanya mabo mengi katika kuboresha sekta ya mawasiliano nchini ikiwemo kukua kwa mtandao huo na kuwa na wateja zaidi ya milioni 12 na kuanzishwa kwa huduma ya M-PESA ambayo inatumiwa na wananchi wengi Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zenye watumiaji wengi kwenye huduma hii kwenye makampuni ya Vodacom Group.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akiongea na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wa hafla fupi ya kujitambulisha kwao iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akiongea na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wa hafla fupi ya kujitambulisha kwao iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam,Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo aliyemaliza muda wake, Rene Meza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania aliyemaliza muda wake, Rene Meza(kulia)akimtambulisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kampuni hiyo, Ian Ferrao kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wa hafla fupi ya kumtambulisha kwao iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Vodacom Tanzania Announces 
New Managing Director
 Vodacom Tanzania Limited today announced the appointment of  Ian Ferrao  as the new Managing Director of the company. He replaces Rene Meza who is moving on to assume the position of Chief Executive Officer of Ooredoo Myanmar on September 1, 2015.
Ferrao is currently the Managing Director of Vodacom Lesotho.  He has over 10 years international experience in Europe and Africa and has held senior leadership positions in various technology  businesses.  Prior to Vodacom Lesotho, he was the Chief Commercial Officer for Vodacom Business Africa and before that he was the commercial director and a shareholder at AfriConnect Zambia. Ferrao’s move to Tanzania is a homecoming of sorts – his grandfather emigrated to Tanzania in 1952 and some of his family members were born in Dar es Salaam, before relocating to the UK in 1970. 
The new Vodacom MD is in his own words, “ a passionate telecoms leader who enjoys creating positive change. I believe that our industry plays a transformational role in the communities in which we operate - we are not simply just about connecting people. Our products & services change lives, create brand new opportunities and make the world a better place. 
I am a firm believer that technological innovation moves the world forward and Tanzania cannot be left behind. We are entering an era where being connected is now a necessity, and we as Vodacom Tanzania have a massive role to play in ensuring all Tanzanians can access the internet, enjoy digital content and create a brighter future for both themselves and the Country.”
For his part, Meza joined joined Vodacom Tanzania in October 2011 as Managing Director. He introduced many firsts in the telecoms sector in Tanzania during his tenure. 
Meza’s most notable achievements include the fact that under his leadership; the network doubled in size,  customer  numbers rose  to over 12 million and Tanzania went on to become the biggest M-PESA customer base in the Vodacom Group.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...