Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA),Eliud Sanga ( kati kati) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa(LAPF), akibadilishana mawanzo na Katibu mkuu wa TSSA, Meshack Bandawe, ( kulia) ambaye pia ni Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa , Augosti 24, mwaka huu mjini Morogoro baada ya mwenyekiti huyo kufungua mafunzo kwa wafanyakazi wa mbalimbali wa mifuko yote ya hifadhi ya jamii chini inayounda Jumuiya hiyo ( kushoto) ni Ofisa Matekelezo wa Mfuko wa PSPF Makao makuu Dar es Salaam.
Na John Nditi, Morogoro
JUMUIYA ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) umewataka vijana wanaoajiriwa katika mifuko inayounda jumuiya hiyo kuingiza mawazo mapya ya ubunifu katika kubuni mbinu mbadala za vivutio ili kukubalika katika soko katika maeneo ya vijijini ambako huduma hizo hazijawafikia watu wengi.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa TSSA, Eliud Sanga , Augosti 24,mwaka huu , wakati alipofungua mafunzo ya siku tano kwa wafanyakazi mbalimbali wa kutoka mifuko yote ya hifadhi ya jamii chini inayounda Jumuiya hiyo .
Alisema kuwa, soko bado ni kubwa la kutatafuta wanachama walio nje ya ajira isiyorasmi kuwaingiza katika mifuko hiyo hivyo ni vyema wakaanza kuelekeza nguvu zao katika kutafuta wanachama maeneo ya vijijini ambako kuna idadi kubwa ya wananchi wanaohitaji huduma zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...