Mhe.
Shaban Ali Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (katikati) akitoa
neno la utangulizi katika Semina ya Mafunzo elekezi kwa Wahe. Majaji wapya wa
Mahakama Kuu ya Tanzania walioapishwa hivi karibuni, aliyeketi kushoto ni Mhe.
Anold Nsekela, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani (T) kulia ni Mhe. Salvatory
Bongole, Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Mhe.
Jaji Ferdinand Wambali (aliyesimama), Mkuu wa Chuo cha Mahakama Lushoto (IJA),akitoa mada juu ya utendaji
kazi katika Mahakama katika mafunzo yaliyoanza kufanyika mapema leo katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Mhe. Shaban Ali Lila,
Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania (katikati) Mhe. Anold Nsekela, Jaji
Mstaafu wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe. Salvatory Bongole, Kaimu Jaji
Mfawidhi-Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na
Wahe. Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania walioapishwa hivi karibuni,
Majaji hao wapo katika mafunzo elekezi yenye lengo la kuwawezesha sheria
mbalimbali na taratibu za Kimahakama. Mafunzo haya yataendelea kufanyika katika
Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA) kuanzia tarehe 24.08.2015 ambapo
mada mbalimbali zitatolewa ili kuwawezesha Wahe. Majaji hao kuifahamu Mahakama,
ikiwa ni pamoja na misingi na taratibu
za utoaji huduma ya haki nchini. (Picha na Mahakama).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...