Walimu wa Shule ya Msingi Muhimbili wakifurahia kupewa viti vipya pamoja na meza na wanafunzi wao waliohitimu shule ya msingi mwaka 1988 katika shule hiyo, wamekabidhiwa Samani hizo leo katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Muhimbili, Dafrosa Assenga akipeana mkono na Mgeni Rasmi Balozi Kassimu Mwawado, mara baada ya kukabidhiwa kiti na meza Mpya kutoka kwa wanafunzi waliohitimu katika shule hiyo Mwaka 1988, ikiwa ni mchango wao katika kuendeleza elimu katika shule hiyo.Kutoka kulia ni Mhitimu wa shule ya msingi Muhimbili mwaka 1988 na Mkurugenzi wa Galaxy Cargo, Jonatha Kasesele, Mwenyekiti wa wahitimu 1988 shule ya msingi muhimbili,Usia Nkoma
Mwalimu mstaafu katika shule ya msingi Muhimbili wa mwaka 1972-2012, Amani Ndussy na Mwenyekiti wa bodi shule ya msingi Muhimbili, George Ntevi.
Mwalimu mstaafu katika shule ya msingi Muhimbili wa mwaka 1972-2012, Amani Ndussy na Mwenyekiti wa bodi shule ya msingi Muhimbili, George Ntevi.
Mwalimu wa shule ya msingi Muhimbili wa mwaka 1986 hadi sasa, Marry Massawe akiwashukuru wanafunzi waliosoma shule hiyo kwa kuikumbuka shule yao.
Wanafunzi wa shule ya msingi Muhimmbili mwaka huu wakiwa wamehudhulia hafra fupi ya wahitimu wa shule hiyo mwaka 1988 leo jijini Dra es Salaam.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
''hafra'', ''hudhuliwa'' hapa walimu wa Mbuyuni shule ya msingi mnabidi mkazie wanafunzi wa miaka hii kuandika maneno ya Kiswahili kwa usahihi.
ReplyDeleteSijui mwandishi wa habari hii ya kutia moyo ni wale LY 1988 hivyo pia wasisitize wanafunzi na walimu kuandika maneneo ya lugha ya Kiswahili kwa ufasaha.
Mwisho natoa hongera kwa wahitimu wa shule ya msingi Mbuyuni mwaka 1988 kwa kujali ubora wa mazingira ya kufundishia wanafunzi wa miaka hii.
waliomaliza uhuru mchanganyiko mwaka 1993..Tuwasiliane tukafanye kitu kama hicho..na wale wa mkwawa 2000..tuwasiliane
ReplyDeleteJAMANI WAWEKEENI WALIMU VITI VYA KIOFISI ACHANENI NA MAMBAO????? ILA HONGERENI JAPO KWA KUKUMBUKA MLIPOTOKA
ReplyDeleteSafi sana kwa wote mlio jitolea kufanikisha shughili hiyo ! Shukran pia zikufikie anko michuzi kwahutuunganisha na matukio yote hasa hasa yahuko nyumbani ! Mimi binafsi
ReplyDeletenimefarijika kumuona mwanafunzi mwenzangu wa sekondari ya Azania 1992
Jonathan Kasesela, Tulikua yunamuita Jobaka ! Nimefulahi sana kumuona akiwa pamoja nawenzake kufanya mambo kama haya! Safi sana jobaka ‐mdau kutoka japan !
kutoka kwa Zakia George
ReplyDeleteMimi pia ni mwanafunzi wa mwaka 1988 Muhimbili primary school. Nimefurahishwa sana na wanafunzi waliojitolea michango kwa kuboresha shule yao waliyosoma. Hongera, Namkumbuka sana Jobaka, he is a funy guy.
Mimi pia nilimaliza masomo shule ya Muhimbili mwaka 1988
ReplyDeleteHongera kwa wote mliyojitolea kukumbuka mliposoma (muhimbili primary school) na mimi pia nimefurahi kumwona Jobaka, he is a funy guy.
From Zakia George