Ni siku ya 14 ambapo mampema kabisa washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015 linaloendeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow na yenye kauli yake ya Wekeza kwa wakulima wadogo wadogo wanawake inalipa , na Kipindi ambacho kinaruka katika Runinga yako kupitia Chanel ya ITV kuanzia saa 12:30 jioni na Marudio saa 11:30 za asubuhi , Katika siku hii Mama Shujaa wa Chakula wanatoka na kuelekea mabondeni kufuata udongo wa Mfinyanzi kwa ajili ya kuja kutengeneza vitu mbalimbali kama majiko, Mifuniko, Mabanda, mapambo, Vyungu na vitu vyengine vingi. 

Ilikuwa ni Safari ndefu ya kufuata udongo huo lakini hatimaye walifanikiwa kuupata na baadae kurudi katika Kijiji chao cha Kisanga na kuanza kutengeneza vitu hivyo na baadae kuwauzia wanakijiji wa Kijiji cha Kisanga.

Pia hii ilikuwa ni nafasi kubwa na ya kipekee kwa Washiriki hao wa Shindano la mama Shujaa wa Chakula kuuza vitu vyao ambavyo walitengeneza wakiwa kwao pamoja na Bidhaa mbalimbali kwa wakazi wa Kijiji cha Kisanga... Hivi ndivyo ilivyokuwa.
 Mama Shujaa wa Chakula wakiwa wanaelekea Bondeni katika kijiji cha Kisanga kufuata udongo wa Mfinyanzi kwa ajili ya kutengeneza vitu mbalimbali ambavyo viliwasaidia kupata kipato.
 Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015 Shindano linalo endeshwa na Oxfam kupitia Kampeni yake ya Grow wakiwa wanachimba udongo wa Mfinyanzi kwa ajili ya kwenda kutengeneza vitu mbalimbali ambavyo baadae waliviuza
 Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 msimu wa nne wakiwa wanamalizia kuchimba udongo
 Kazi imeanza ambapo washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula linalo endeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow na Kurushwa katika Runinga yako kupitia Chanel ya ITV kuanzia saa 12:30 za jioni na Kurudiwa saa 11:30 asubuhi wakiwa bize kila mtu kufinyanga vitu mbalimbali.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tanzania imebarikiwa na ardhi nzuri yenye rutuba kazi kwetu kuiendeleza ili ituendeleze.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...