Waziri Mkuu mstaafu, Fredreck Sumaye (kushoto), akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo mchana.
Waziri Mkuu mstaafu, Fredreck Sumaye (kulia), akipeana mkono na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe Dar es Salaam leo mchana, baada ya kujiunga na chama hicho. Anayeshuhudia katikati ni Mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Sumaye akisisitiza jambo
Sumaye (wa tatu kulia), akiwa na viongozi wanaunda Umoja wa Katiba (UKAWA) baada ya kuondoka CCM na kujiunga na Chadema. PICHA NA HABARI ZA JAMII BLOG
ni ukomavu wa demokrasia kwani watu hata dini wanabadili.
ReplyDeletekitu ambacho sijaelewa ni kwa vipi mtu anajiunga na 'UKAWA' sababu ukawa si chama na hakina kadi. angetakiwa kwanza ajiunge na chama funali kinachounda huo UKAWA
Nami nilijiuliza same question ila nadhani amejiunga na ukawa through chadena kama alivyofanya lowasa
Deletekaskazini wamejipanga ...
ReplyDeleteKama Sumaye alivyosema anajiunga na UKAWA ila kuhusu chama alichojiunga atafahamisha baadaye kama umemsikiliza........ watu wengi wamehamia CHADEMA si wa kaskazini pekee bali na sehemu nyingine za nchi. Mbona wengi tu wa kaskazini hawajahama kama vile KINANA na kina Msuya? Acheni hayo mambo ya kuhalalisha ukabila....mbona hamsemi sehemu zingine kama Lindi, Mtwara, Singida, Tabora, Songea, Tanga n.k ambazo ni sehemu (strongholds za CCM) na watu hawalalamiki.
ReplyDeleteFredi ameweka wazi kwamba anahamia upinzani ili kuiimarisha CCM.
ReplyDeleteEdo inafahamika kwamba ameenda kuharibu kazi iliyofanywa miaka yote ya upinzani. Huwezi kuwa fisadi hapo Mwembe Yanga halafu ghafla ukatakata kwa vile tu umejiunga na waliokuita fisadi.
Kajiunga NCCR sio CDM
ReplyDeleteMZEE WANGU SUMAYE PUMZIKA KWA AMANI WAPISHENI VIJANA WAFANYE KAZI SASA …… NG'OMBE HANENEPI CK YA MNADA HATA MARA MOJA . ULITAKIWA KUTOKA CCM MAPEMA KABLA HATA YA KUOMBA NAFASI YA URAISI . SS VYOOTE UMESHINDWA NA HUKUJIANDAA VIZURI LEO CC TUNAANXA SHUGHULI NAMBA UTAISOMA VIZURI SAFARI HII . UNAMUANA MZEE WANGU MSUYA AMEKAA PEMBENI TU AMEWAACHIA VIJANA WAFANYE KAZI . KAULI ULIYOTUMIA ETI DEMOKRASIA YA KWELI NI MPAKA UWE NJE YA CCM SIYO SAHIHI KWANI HAINDANI NA WAKATI ULIOPO . HIVI WW UKIGOMBANA NA MKEO UTAKIMBIA NJE UKALALE NA CHANGU NJE COZ UMESHINDWA KUELEWANA NA MKEO NDANI YA NYUMBA . SASA KAMA YA NDANI TU YAMEKUSHINDA TUKIKUPA MAGOGONI JE SI NDIO UTAKUWA KICHUROOO . KIRERUUUUUU …… NGACHOKA
ReplyDeleteDuniani watu hawafanani kabisa, kila mtu anao mtazamo, hisia, lengo na dhamira yake. Mfano,waweza kumtembelea rafiki yako, ukaona jinsi mke wake anavyojibizana na mme wake, ukasema rohoni, mmm angekuwa mke wangu namtimua...lakini rafiki yako ukamuona ametulia akifokewa....hiyo taasisi Yao...wewe Ni mgeni. Tusiwe tuna jumla mipango na malengo ya kila mtu.!!!
DeleteMNASHANGAA NINI?????? UKAWA WAMESHAONA LOWASSA HAWEZI KUSIMAMA ZAIDI YA DAKIKA 20 KUHUTUBIA NA KWA KUWA AFYA YAKE MGOGORO NJIA RAHISI KUMTAFUTA MBADALA WA KUMSAIDIA,HIVI KWELI LOWASSA AKIWA RAIS ATAWEZA KUKAGUA GWARIDE PALE UWANJA WA TAIFA??? WAPIGA KULA ANGALIENI SI KILA KING'AACHO NI DHAHABU,HII KALI YA UCHAGUZI WA MWAKA HUU HUYU HUYU SUMAYE ALIWAHI KUSEMA KUWA LOWASSA NI FISADI MKUBWA NA AKICHAGULIWA CCM KAMA MGOMBEA ATARUDISHA KADI ATAJIONDOA SASA KIPO WAPI??????????????????????????
ReplyDeleteunapotoa maoni yako huku ukizingatia yeye Sumaye ni dini gani au kabila gani basi ujue kuwa inawezekana kuwa WEWE ndio mdini au mkabila na si YEYE Sumaye. Hivyo badili mawazo yako.
ReplyDeleteMimi sijui huyo ni dini au kabila gani ila najua akiwahi kuwa waziri mkuu.
ReplyDeleteMbona hakuna anayetabasamu?
Why long faces?
Mie haya ya kuhama yananifurahisha kwani yanaonesha uwazi wa kujaribu kushindana. Kwa TZ yanatushangaza ila Mzee Mandela aliwahi kusema- "Mara zote uonekana haiwezekani mpaka hapo inapoweza kufanyika". Sasa inafanyika...PMs wanahamia upinzani, Mie sikutegemea...mtu aliyewahi kuwa Waziri Mkuu...ni mtu mkubwa Sana!!! Angalau, wanatimiza hali Yao ya kikatiba kuliko km wangekwenda msituni...vita..nk km tunavyoona kwingine!!! Serikali yetu isisimamie mechi hii, Ili tuweke historia ktk demokrasia Tanzania. Tusipoteze muda kuwajadili watu, tujadili mchakato, tukijikita kwenye hali ya hali na utii wa sheria,kanuni na taratibu za kuufanya uchaguzi!!! Haya ya ukabila, sehemu, ukanda, dini tuyaaache hapo twajua hapo na yanatumika kichini chini na WAJINGA.
ReplyDelete