Akiendelea na ziara katika Mamlaka zinazohusu udhibiti wa huduma za kiuchumi na za kijamii,Waziri wa Nchi(Kazi Maalum), Ofisi ya Rais,Profesa Mark Mwandosya ametembelea makao makuu ya Tume ya Ushindani wa Haki kibiashara, na Baraza la Ushindani, Ubungo, Dar es Salaam.
Tume ya Ushindani(Fair Competition Commission-FCC) imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003. Madhumuni makubwa ya uwepo wa Tume ni kukuza na kulinda ushindani wa haki katika biashara na kumlinda mtumiaji wa bidhaa na huduma dhidi ya mwenendo usiofaa katika soko. Baraza la Ushindani,ambalo ni baraza la rufaa nalo limeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003 ili kusikiliza na kutoa maamuzi ya kesi zinazohusu masuala ya ushindani.
Akiongozana na maafisa waandamizi kutoka vyombo vya udhibiti vya kisekta, SUMATRA, TCAA, TIRA, na EWURA, Waziri Mwandosya alipata taarifa za utendaji na kuzungumza na watendaji wa FCC na FCT kuhusu mafanikio na changamoto, namna ya kukabili changamoto hizo ili kuzifanya taasisi za udhibiti zichangie vilivyo katika kukuza uchumi.
Katika picha ya kwanza waliokaa, kushoto ni Dr Frederick Ringo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani. Katikati ni Waziri Mwandosya, na kulia ni Ndugu Paul Ngwembe,Mkurugenzi wa Sheria, Mamlaka ya Udhibiti wa sekta ya Bima. Wengine ni maafisa wa Tume,na wawakilishi wa mamlaka za udhibiti za kisekta.
Katika picha ya pili, Profesa Mwandosya ,katikati,akiwa na Ndugu Kunda Mkenda,Kaimu Msajili wa Baraza la Ushindani,kulia kwake, pamoja na maafisa watendaji wa Baraza na kutoka mamlaka za udhibiti za kisekta.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...