Jitihada
za serikali katika kupambana na uhalifu wa mitandao imeungwa mkono kutokana na
baadhi ya vyuo kuanzisha mitaala yenye somo la ulinzi wa mitandao.
Moja
ya jitihada za serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo ni kupeleka
muswada wa kutunga sheria ya uhalifu wa mtandao ya mwaka 2015 katika mkutano wa 19 wa bunge la jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania ambao ulipitishwa na bunge hilo.
Taarifa
ya waziri wa Mawasiliano , Sayansi na Teknologia , Profesa Makame Mbarawa
kuhusu sheria hiyo inasema kukua kwa kasi kwa matumizi ya Teknolojia ya Habarina
Mawasiliano (TEHAMA) kumeleta mafanikio ya kwa kuongezeka kwa huduma za
mawasiliano, huduma za kifedha na matumizi ya mitandao ya kijamii.
Aidha,
mafanikio hayo yameleta changamoto nyingi
katika
jamii ikiwemo kuibuka kwa makosa mapya ya
jinai na pia
mbinu
mpya za kutenda makosa ya zamani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...