Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Michael John akizungumza juu ya Upungufu wa vitamini na Baadhi ya Madini muhimu kama Vitamini A, folate, Madini chuma Zinki na madini joto ni chazo cha vifo kwa Watoto chini ya miaka Mitano na chanzo kikubwa cha maradhi mbalimbali kote Duniani, kulia ni Mkurungenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Alliance for Iproved Nutrition (GAIN) ,Marc van Amerngen katika mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mkurungenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Alliance for Iproved Nutrition (GAIN), Marc van Amerngen akizungumza na waaandishi wa habari hawapo pichani juu ya Kongamano la kimataifa litakalofanyika jiji Arusha Septemba 9-10 mwaka huu katika mkutano uliofanyika leo Jiji Dar es Salaam kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Michael John.
Mkurungenzi Msaidizi huduma za lishe Dr.Vincent Asey kuliani Dr. Generose Mulokozi akizungumza juu ya Matatizo ya lishe yanamgusa kila mmoja wetu kote Duniani katika mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandish wa habari walio hudhulia mkutano huo jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Emmanue Massaka.
TAKWIMU zinaonyesha zaidi ya watoto milioni 3.1
wenye umri chini ya miaka mitano hufariki Dunia kila Mwaka huku wengine Milioni
161 kupata matatizo ya kudumaa mwili kutokana na kukosekana kwa virutubisho vya
chakula.
Madhara hayo
yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuongeza virutubisho kwenye vyakula
ikiwemo Unga,Mafuta ya kula pamoja na Chumvi.
Hayo yalisemwa
leo jijini Dar es salaam na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Michael Jonh wakati wa mkutano na
waandishi wa habari ikiwa lengo ni kutoa tamko kuhusu Kongamano la kimataifa la
Urutubishaji Chakula litakalo septemba 9 hadi 11 mwaka huu jijini Arusha.
Aidha amesema
kuwa Chanzo cha Vifo hivyo ni upungufu wa vitamini pamoja na dbaadhi ya madini
muhimu kama vile vitamin A,Folate,Madini Chuma,Zinki na Madini Joto hali
inayosababisha maradhi mbalimbali katika maeneo mengi duniani.
Kwa upande
wake Mkurugezi Msaidizi wa huduma za lishe kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii Vicent Assey alisesema kuwa
utafiti wa mwaka 2010 umebainisha asilimia 42
ya watoto ni walemavu kutokana na Lishe Duni.
Alisema kuwa
nchi ambazo zimeathirika na tatizo la
vifo kwa watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano kutokana na ukosefu wa
virutubisho kwenye chakula ni zile ambazo zipo kusini mwa jangwa la sahara
Barani Afrika.
Alizitaja
nchi hizo kuwa ni pamoja na Tanzania ambayo ipo nafasi ya tatu kulingana na
takwimu za vifo kwa watoto ,huku DRC
Kongo ikishika nafasi ya pili, na Ethiopia ikiwa ni ya kwanza kutokana na sababu kubwa ya kukumbwa na migogoro ya kivita katika nchi
hizo.
Kutokana na
changamoto hizo Serikali ya Tanzania kwa Kushirikiana na Shirika la masuala ya
urutubishi wa chakula duniani la Global Alliance For Improved Nutrition (GAIN) inatarajiwa
kuwa mwenyeji wa kongamano hilo la kwanza la kimataifa ambalo shabaha yake
kubwa ni kuzungumzia masuala ya urutubishaji chakula.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...