Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
BENKI ya DCB imekutanisha viongozi
wa mifuko ya kuweka na Kukopa (SACCOS)
kuweza kuwapa fursa mbalimbali zilizopo katika benki hiyo.
Akizungumza na viongozi wa SACCOS,Meneja
Mwandamizi wa Biashara Ndogo na Kubwa,Haika Machaku,amesema benki ya DCB iko
karibu na SACCOS katika kupata fursa za utuzaji wa Amaana na huduma mbalimbali
kwa gharama nafuu.
Amesema wataendelea kushirikiana na SACCOs kuangalia watavyoweza kusaidiana
katika kuimarisha saccos pamoja na wanachama kunufaika na mikopo katika benki
hiyo.
Aidha amesema kuwa nia ya benki kuahakikisha wanachama
wananufaika na benki katika kuendeleza
maisha kupitia fursa ambazo benki imeanisha kuinua wajasiriamali pamoja na ushirika ikiwemo SACCOS.
Benki imewataka viongozi wa
SACCOs kufungua akaunti katika benki
hiyo katika kuweza kuanza kufanya kazi
kwa ushirikiano na fursa zao ziweze kuwafikia wanachama.
Meneja wa Mwandamizi wa Biashara Ndogo
na Kubwa wa Benki ya DCB,Machaku,akizungumza na viongozi mbalimbali wa Saccos
juu ya fursa zinazopatikana katika benki
ya DCB leo Makao Makuu ya DCB jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Benki ya DCB, Boyd
Mwaisame akizungumza na viongozi wa SACCCOs jinsi watavyoshirikiana katika kuinua SACCOs,leo
Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa SACCOS ya
Wafanyakazi wa TRL,Gwammy Mwakangale Akichangia maada katika mkutano wa
DCB juu ya faida zinaziopatikana katika
benki hususani mikopo ya nyumba leo Makao Makuu ya DCB,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki ya viongozi wa SACCOs wakiwa katika mkutano
ulioitishwa na benki ya DCB kuwapa fursa zinazopatikana katika benki hiyo leo
jijini Dar es Salaam.
picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...