Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Washington DC, Kalley Pandukizi  (kulia) akiwa na Katibu wa chama hicho, Ndugu Libe Mwang'ombe (katikati) alipotoa kadi rasmi kwa Beautician maarufu na designer Mtanzania, Linda Bezuidenhout (kushoto). Picha ya Maktaba.

Napenda kuchukua nafasi hii kukanusha taarifa ya uongo na uzushi iliyoenezwa kupitia mitandao ya kijamii leo tarehe 18 Septemba 2015 iliyoanzia kwenye JamiiForums yenye kichwa cha habari “Mbowe asalimu amri kwa Dr Slaa”. Katika taarifa hiyo mwandishi amenitaja mimi Kalley Pandukizi kama mmoja wa viongozi wa CHADEMA tawi la DMV pamoja na viongozi wenzangu kuwa tumewapokea viongozi hao wa juu hapa Marekani na wapo katika hoteli moja Ohio kwa ajili ya mazungumzo binafsi.


Napenda kueleza umma kuwa taarifa hii si ya kweli, ni ya uongo na uzushi yenye lengo la kuhadaa umma wa Watanzania kuwa kuna mazungumzo kati ya viongozi hawa hapa Marekani. Pia ina lengo la kunichafulia jina mimi kama Mwenyekiti wa CHADEMA tawi la DMV.

Mwisho napenda kutoa wito kwa wanachama na wapenzi wa CHADEMA pamoja na UKAWA kwa ujumla wake, kupuuzia taarifa kama hizi zenye lengo la kupotosha na kuhadaa umma kwa malengo mabaya ya kisiasa, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.

Imetolewa na:-
Mwenyekiti wa CHADEMA - DMV, Marekani
Kalley Ammy Pandukizi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...