Ni neema kubwa ambayo
imepatikana kwa juhudi kubwa zilizofanywa na viongozi wakishirikiana na wana
jamii pamoja na mambo mengine lakini kuhakikisha jamii inakuwa pamoja.
Kipaumbele cha mwanzo ikiwa
kuwafundisha vijana na wazee maadili mazuri, aidha kujenga moyo wa kushirikiana
na kuhakikisha umoja wenye afya. Ni bahati kubwa kwa watu wa ughaibuni kuweza
kukutana ktk mji mmoja wakiwa wanazugumza lugha moja, utamaduni wao mmoja na
wana maadili yanayofanana.
Ili kuona kwamba hayo yanafanikiwa wameandaa sherehe
ya siku mbili tarehe 24 na 26/09/2015 kuanzia saa nane mchana hadi saa nne usiku.
Vyakula vya ki-asili kama vile urojo,mishikaki na vinginevyo vitauzwa kwa
malengo ya kuiingizia jumuiya mapato ili kufanikisha malengo wanayo yakusudia.
Kutakua na kiingilio £ 10 kwa familia moja na £5 kwa wasio hudhuria na familia.
Tunawatakiwa Eid njema na tunasema: Eid Mubaarak.
Kwa kutaka kuifahamu vizuri COMSWA na
kazi zake tembelea www.comswa.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...