Wanachama wa CCM Wakimshangilia Mgombea wao wa Urais Dk Shein, wakati akiwasili katika viwanja vya mpira Konde kwa ajili ya mkutano wake wa Tatu wa Kampeni zake kisiwani Pemba.
Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein, akionesha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Wananchi wa Wilaya ya Micheweni Pemba wakati wa mkutano wake wa Kampeni na kuwataka kuichagua CCM kuzi kuwaletea maendeleo katika miradi mbalimbali na kuendelea kuongoza Zanzibarb kwa misingi ya Sheria na haki kwa maendeleo ya Wazanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk. Shein akiwatambulisha Wagombea Udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi katika Wilaya ya Micheweni Pemba wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar katika viwanja vya mpira Konde Pemba. 
Wananchi wakishangilia wakati wa kuwatambulisha wagombea Ubunge na Uwakilishi na Udiwani wa Wilaya ya Micheweni Pemba.
Shekh akisoma dua baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni ya Urais wa Zanzibar uliofanyika kastika viwanja vya mpira Konde Pemba Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba. Picha zaidi BOFYA HAPA



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Serikali ya umoja wa kitaifa iendelee imeleta amani na utengamano visiwani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...