CHAMA cha soka
mkoa wa Dar es salaam, DRFA kwa kushirikiana na shirikisho la soka nchini
TFF,leo imezindua rasmi kozi ya ukocha wa leseni C’ inayotambuliwa na
shirikisho la kandanda barani afrika CAF.
Kozi hiyo ya
wiki mbili inaendeshwa na mkufunzi, Salum Madadi ambaye ni mkurugenzi wa ufundi
wa TFF,ikiwa na jumla ya washiriki 31 wengi wao wakiwemo makocha wa vilabu vya
ligi daraja la pili,daraja la kwanza na ligi kuu.
Miongoni mwa
washiriki hao ni pamoja na kocha msaidizi wa Simba,Suleiman Matola,katibu mkuu
wa zamani wa Simba Muhina Kaduguda,kocha wa Ruvu shooting Tom Olaba,kocha wa
makipa wa Yanga Juma Pondamali,nyota wa zamani wa Taifa Stars, Ally Mayai na
Peter Tino.
Mgeni rasmi
katika ufunguzi wa kozi hiyo ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF,Msafiri
Mgoy,ambaye amewapongeza washiriki kwa uamuzi wao wa kutaka kujiongezea maarifa
ya ufundishaji wa soka ,kwa kuwa tanzania inakabiliwa na upungufu mkubwa wa
makocha ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika ambayo yamepiga hatua
kisoka.
Aidha amesema TFF imeweka mpango maalum wa kutunza kumbukumbu za makocha hao na wengine
watakaopatikana,pamoja na kufuatilia kazi zao kwenye vilabu mbalimbali
watakavyofundisha ili iwe rahisi kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanya
kazi zao.
Naye mwenyekiti
wa DRFA,Almasi Kasongo wakati akimkaribisha mgeni rasmi,amesema chama chake
kinataraji pia kuendesha kozi za madaktari pamoja na kuendeleza mpango wake wa
kuinua soka la vijana,ili taifa liwe na wachezaji wenye uwezo wa kushindana na
mataifa mengine.
Kasongo
amesema licha ya chama chake kuwa na mikakati ya kuhakikisha soka la mkoa wa
Dar es salaam na nchi kwa ujumla linanyanyuka,lakini bado nguvu kumbwa
inahitajika kutoka TFF pamoja na wadau wenye mapenzi mema na mpira wa nchi hii.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI NA
MAWASILIANO YA DRFA,
Omary Katanga,
Mkuu wa habari na mawasiliano DRFA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...