Flyer by Evelina Moceviciute 2015 
Mwanamuziki mkazi London, Freddy Macha, anatazamiwa kutumbuiza kwa ngoma na muziki wa gitaa, kwenye tafrija ndogo kutangaza na kuuza picha za watoto wa Kitanzania. Tafrija na maonesho yametayarishwa na wapiga picha watatu wa Kizungu, Amy Read, Evelina Moceviciute na Saraya Cortaville waliofanya kazi za kujitolea Mbeya vijijini mapema mwaka huu. 
Mauzo ya taswira hizo yatatumika kusaidia maisha na elimu ya watoto hao hao waliopigwa picha. Mradi mzima unaitwa "Ahsante Children"...kutukuza na kutangaza lugha ya Kiswahili, Tanzania na wananchi Afrika Mashariki. 

Onesho litafanywa katika mkahawa wa:

The Chapel St Margaret's House, 
21 Old Ford House, 
Bethnal Green, 
Hackney, London E2 9PL. 
Jumapili 4 Oktoba 2015. Saa 11 na nusu jioni hadi 3 usiku. 
HABARI ZAIDI www.freddymacha.com/ Freddy Drums - Germany May 2012- pic by Luis Tome Passarello 
Freddy Macha na ngoma. Picha ya Luis Tome Passarello

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...