President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete delivers his keynote speech during the 10th Africa Travel Association Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center in United States of America this morning.
Some of the delegates to the 10th ATA Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center in United States of America this morning.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with the Minister for Natural Resources and Toursim Hon. Lazaro Nyalandu during the 10th Africa Travel Association Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center.
The Director Africa House and Economics Professor at the New York University Yaw Nyariko presents souvenir gift to President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete during the 10th Annual Presidential Forum on Tourism held at New York University Kimmel Center in New York this morning. Center is the Minister for Tourism and Natural Resources Hon. Lazaro Nyalandu.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in a group photo with panelists and coordinators of the ATA 10th Annual Presidential Forum on Tourism held at at New York University Kimmel Center in United States of America this morning. From left Executive Director Africa Travel Association(ATA) Mr. Edward Bergman, Namibia’s Minister for Environment and Tourism Hon. Pohamba Shifeta,(second left), Kenya’s Cabinet Secretary in the Ministry of East African Affairs, Commerce and Tourism Hon. Phyllis Kandie(Third left), Mali’s Minister for Culture, Crafts and Tourism Hon. N’Diaye Ramatoulaye Diallo(fourth left),The President, The Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro Nyalandu, Director Africa House and Professor of Economics Dr. Yaw Nyarko(seventh left), ), Uganda’s Minister for Tourism Wildlife and Antiquities Hon.Dr. Maria Mutagamba,(eight left) and the panel moderator who is also the CBS News Travel Editor Mr. Peter Greenberg(photos by Freddy Maro)
-------------------------------------------------------------------
Rais
Kikwete afafanua changamoto za utaalii wa Afrika
·
Asema
habari hasi kuhusu Afrika zinavuruga utalii wa Afrika
·
Asisitiza
Tanzania itaendelea kupambana na ujangili
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameelezea changamoto
kubwa zinazozuia kukua haraka zaidi kwa sekta ya utalii katika Afrika na hivyo
kuliwezesha Bara hilo kuchuma matunda makubwa zaidi kutokana na sekta hiyo.
Aidha, Rais Kikwete
amesema kuwa pamoja na kuwa na vivutio vingi vya utalii, Bara la Afrika, bado
linabakia nyuma kwa kiasi kikubwa katika kuvutia watalii wa kimataifa na katika
mapato yanayotokana na utalii.
Rais Kikwete vile
vile amesema kuwa Tanzania itaendelea kutenga eneo kubwa la ardhi yake kwa
ajili ya hifadhi na pia itaendelea kukabiliana na ujangili dhidi ya tembo,
ambao hata hivyo amesema kuwa umepungua katika mwaka uliopita.
Rais Kikwete
ameyasema hayo leo, Alhamisi, Septemba 24 wakati alipotoa hotuba ya ufunguzi wa
shughuli za Miaka 10 ya Chama cha Usafiri cha Afrika – Africa Travel Association (ATA)
na Miaka 10 ya Jukwaa ya Rais Kuhusu Utalii – Presidential Forum on Tourism
kwenye Kituo cha Kimmel cha Chuo Kikuu cha New York (New York University Kimmel
Center) Africa House, mjini New York.
Rais Kikwete yuko New
York, Marekani kwa ajili ya kuhudhuria shughuli za mwaka huu za Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa (UNGA) baada ya kumaliza kuendesha vikao vya Jopo la Watu
Mashuhuri Duniani ambao wanatafuta jinsi gani dunia inavyoweza kujiandaa vizuri
zaidi kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ambavyo pia vilifanyika New York.
Rais Kikwete ametambulishwa
na kukaribishwa kutoa hotuba yake na Dkt. Yaw Nyarko, Raia wa Ghana na
Mkurugenzi wa Africa House ambaye pia ni Profesa wa Uchumi kwenye Chuo Kikuu
cha New York na Bwana Edward Bergman, Mkurugenzi Mtendaji Mwanzilishi wa ATA.
Alikuwa ni Rais
Kikwete na familia ya Bergman ya New York ambao walianzisha na kujadili wazo la
kuanzishwa kwa chama hicho miaka 10
iliyopita.
Kabla ya kutoa hotuba
yake, washiriki wa Kumbukumbu hiyo ya miaka 10 wamesikia maelezo ya kina kutoka
kwa mawaziri wa nchi tano za Afrika kuhusu hali ya utalii katika nchi hizo na
katika Bara la Afrika kwa jumla.
Mawaziri
waliozungumza kwenye shughuli hiyo iliyoendeshwa na Bwana Peter Greenberg,
Mhariri wa Usafiri wa Televisheni ya CBS ni Mheshimiwa Lazaro Nyalandu wa
Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Maria Mutagamba, Waziri wa Utalii, Wanyamapori na
Nyaraka wa Uganda ambaye pia ni Rais wa ATA na Mheshimiwa N’Diaye Ramatoulaye
Diallo, Waziri wa Utamaduni, Utalii na Usanii wa Vinyango wa Mali.
Mawaziri wengine
ambazo wamezungumza katika shughuli hiyo ni Mheshimiwa Phylis Kandie ambaye ni
Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki, Biashara na Utalii wa Kenya na Mheshimiwa
Pohamba Shifeta, Waziri wa Mazingira na Utalii wa Jamhuri ya Namibia.
Akizungumza katika
shughuli hiyo, Rais Kikwete amesema kuwa changamoto kuu zinazokabili maendeleo
ya utalii katika Afrika ni miundombinu ya kitalii, utangazaji wa masoko ya
utalii na matatizo ya usafiri wa anga kuingia na kutoka Afrika.”
“Lakini pia kuna
jambo kubwa la mtazamo hasi kuhusu Afrika. Kwa kawaida, vyombo vya habari vya
nje vinalielezea Bara la Afrika kama Bara hatari ambalo sifa zake kuu ni
migogoro, magonjwa na matatizo yanayotokana na umasikini. Haya yote siyo ya
kweli ni upotoshaji wa makusudi.”
Ameongeza Rais
Kikwete: “Ukweli kuhusu Afrika lazima uelezwe kwa usahihi na sisi wenyewe.
Picha inayojengwa kuwa tatizo katika nchi moja ni tatizo la Bara zima siyo ya
kweli na lazima itafutwe namna ya kulisahihisha jambo hilo. Afrika ni Bara la
nchi 54 na siyo nchi moja ya majimbo 54.”
Ameongeza: “Ni
upotoshaji huu ambao ulisababisha watu kufuta safari za kitalii kwenda Afrika
wakati ugonjwa wa Ebola ulipolipuka katika Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Lakini Zanzibar katika Tanzania ni safari ya saa tisa za ndege kutoka nchi hizo
tatu za Afrika Magharibi. Kwa hakika nchi hizo tatu ziko karibu zaidi na Bara
la Ulaya kuliko ilivyo Kenya. Hili ni tatizo kubwa ambalo lazima lisahihishwe
haraka iwezekanavyo.”
Kuhusu mapato ya
utalii, Rais Kikwete amesema: “Mwaka jana, Afrika ilipokea watalii wa kimataifa
milioni 56 ambalo ni ongezeko la asilimia mbili tu ya watalii wote wa kimataifa
waliotembelea maeneo mbali mbali ya dunia na asilimia tano ya watalii wote
waliotembelea dunia mwaka jana.”
Kuhusu Tanzania, Rais
Kikwete amesema kuwa Tanzania inaendelea kutenga asilimia 36 ya eneo lake lote
kwa ajili ya shughuli za hifadhi.
“Tumefanya hivyo
tokea uhuru wetu. Tutaendelea kufanya hivyo. Kama mnavyojua pia tumekuwa
tunakabiliana na changamoto ya ujangili ambao ulitishia kumaliza idadi ya tembo
wetu. Tumechukua hatua na kuendesha kampeni dhidi ya janga hili. Sasa tunaanza
kuona matunda ya juhudi zetu. Mwaka 2012 walikuwa wanauawa tembo sita kwa
mwezi. Katika mwaka mmoja uliopita, hajauawa tembo yoyote.”
Rais Kikwete pia ameshangiliwa
sana wakati alipowaambia washiriki wa shughuli ya leo: “Napenda kuchukua nafasi
hii, vile vile, kuwaageni marafiki zangu wote wa ATA kwa sababu hotuba hii ni
yangu ya mwisho nikiwa Rais wa nchi yangu. Nitaondoka madarakani baada ya
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, 2015 baada ya kuwa nimekamilisha vipindi
viwili vya uongozi wangu kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...