Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa hotuba kwa Maofisa Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kwenye ufunguzi wa Kongamano la Wasaidizi wa Sheria lililofadhiliwa na Shirika la Envirocare ambapo Kongamano hilo litafanyika kwa siku tatu kuanzia leo Septemba 2, 2015 Mkoani Morogoro.
 Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo ambao ni Maofisa wa Jeshi la Magereza kutoka Mikoa Mitano Tanzania Bara(Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Morogoro) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi ambaye ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja
 Meza Kuu wakimsikiliza Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani - Jeshi la Polisi, Kamisheni ya Upelelezi, Mrakibu wa Polisi Emmy Mkonyi(hayupo pichani). Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma kutoka Wizara ya Sheria na Katiba, Bw. Joseph Ndunguru(kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(katikati) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.

 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimpongeza baada ya kukabidhi  cheti cha kuhitimu Mafunzo ya Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kwa mmoja wa Washiriki wa Kongamano hilo linalofanyika Mkoani Morogoro. 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati) walioketi akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria kutoka Mikoa Mitano ya Magereza Tanzania Bara(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Kato Rugainunula(wa pili kulia) ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Joseph Ndunguru(wa kwanza kushoto) ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi - Jeshi la Polisi, Mrakibu wa Polisi, Emmy Mkonyi(wa pili kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Envirocare, Bi. Loyce Lema(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...