Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete (Pichani)ameridhishwa na Wakala
wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa hatua iliyofikiwa ya kuweza kusajili
jina la biashara kwa njia ya mtandao na kupata cheti ndani ya saa moja.
“Hatua hii ya BRELA ni nzuri, wanastahili
pongezi na wengine waige,” alisema Dkt. Kikwete kwenye mkutano wa Nane wa
Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Pongezi
za Dkt. Kikwete zilikuja wakati wa kipindi cha majadiliano juu ya kuboresha
mazingira ya kufanya biashara nchini ambapo alijulishwa maendeleo hayo na Ofisa
Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Frank Kanyusi.
Akithibitisha
maendeleo hayo mmoja wa washiriki wa mkutano huo kutoka VIBINDO alisema hivi
karibuni aliweza kufanikiwa kusajili jina la biashara kwa kipindi cha saa moja
tu.
BRELA
imeanza mfumo huo wa kusajili jina la biashara kupitia mtandao mwezi Juni mwaka
huu.
Mteja
wa BRELA anayetaka kusajili jina la biashara anatakiwa kuwa na jina analopendekeza,
anuani ya barua pepe, kitambulisho cha taifa, pasi ya kusafiria, kitambulisho
cha kupigia kura au leseni ya gari, namba ya simu na kufahamu tarehe yake ya
kuzaliwa.
Mteja
anatakiwa kuingia katika mtandao wa BRELA ambao ni www.brela.go.tz kisha ataingiza jina na baada
ya jina kukubalika, atapata nyaraka ya malipo yenye namba ya kulipia.
Baada
ya hapo, mteja atachukua namba ya malipo kwenye nyaraka hiyo na kwenda kulipia
benki za NMB au CRDB na baadaye kuingiza namba ya malipo yake katika kumalizia
mchakato huo wa kimtandao.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...