KUNDASAI ROBERT TERRY
16-09-1964 mpaka 16-09-1998
Mume wangu mpendwa, leo umetimiza miaka
kumi na saba(17) tangu ulipoitwa mbinguni kwa Baba.
Hatuna cha kusema, tumebaki kushukuru tuu maana
imeandikwa tushukuru kwa kila jambo. Kweli ua zuri limerudi kwenye bustani ya
Eden.
Tunakumbuka sana upendo wako na utanashati uliokuwa
nao. Kundasai, tupo kama ulivyotuacha kama familia. Imani yetu kuwa ipo siku
wote tutakutana tena paradiso.
Unakumbukwa
sana na mimi mkeo mpendwa Elizabeth,
wanao Harrison na Diana, nduguzo Martha, Hellen, pacha mwenzio Luwera, Alice, Glad,
Vivian na Aida, wajomba wa kwa Terry wote wa mamba kwa Kiria, wa- Kweka wote wa
narumu, majirani wa Temeke- mikoroshini na mtoni kijichi- DSM, ndugu, jamaa na
marafiki wote.
“
RAHA YA MILELE UMPE EEE BWANA............”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...