KWAYA
tatu za muziki wa Injili Tanzania zinatarajia kuwa mojawapo ya wadau
watakaoiombea amani Tanzania kuelekea uchaguzi Mkuu kupitia Tamasha la
Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4.
Kwa mujibu wa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama pamoja na kwaya
hizo maombi hayo ya amani yatashirikisha waimbaji wengine wa Tanzania na
nje.
Msama alizitaja kwaya hizo ni pamoja na Kwaya ya
Uinjilisti ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Kwaya ya Mtakatifu
Andrew Anglican ya Dodoma sambamba na kwaya ya Wakorintho wa pili ya
Mafinga mkoani Njombe.
Msama alisema Watanzania wajiandae
kupata neno la Mungu lenye lengo la kuombea amani nchi yao kupitia
viongozi wa dini na wadau wengine.
"Suala la amani linatakiwa
kuzungumzwa na kila mmoja, hivyo ni wakati wa kuunganisha nguvu pamoja
kwa lengo hilo," alisema Msama.
Msama alisema kamati yake
inaendelea na mchakato wa kufanikisha tamasha hilo ambalo litaunganisha
nguvu kumfikia Mungu kwa maombi.
Aidha Msama alisema baada ya
kumalizika kwa tamasha hilo jijini Dar es Salaam, Oktoba 6 tamasha hilo
litafanyika Morogoro, Oktoba 8 (Iringa), Oktoba 10 (Makambako), Oktoba
11 (Mbeya), Oktoba 13 (Dodoma), Oktoba 14 (Singida), Oktoba 15 (Tabora),
Oktoba 16 (Shinyanga) na Oktoba 18 (Mwanza).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...