Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akinadi sera zake kwa umati wa wakazi wa Mji wa Dodoma waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini humo leo Septemba 11, 2015, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Mikutano yake ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Benson Kigaila, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma leo Septemba 11, 2015.

Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa mji wa Dodoma waliofurika kwa wingi wao kwenye Uwanja wa Barafu mjini humo, kwa ajili ya kusikiliza sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.

Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu akiwaga cheche zake katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma.

KUONA PICHA ZAIDI 
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Naitwa Jongoo, ndugu zangu watanzania na wana Ukawa mimi kama mwana harakati nisiye na chama huku nikiwa kama refarii wa huu mpambano 2015 nime jalibu kuzizoom hizi picha moja baada ya nyingine jibu nikapata wengi wa huu umati ni vijana tena chini ya umri ambao kisheria hawa pigi kula sasa je hapa itakuaje? mimi kama mwana harakati na refarii wa huu mpambano natoa angalizo mapema kwa hii team sitaki lawama baada ya mchezo eti ooo refarii kapendelea wakati nyie wenyewe ndio mmeamua kuchezesha watoto mbele ya manje mba wa ACT Wazalendo na CCM naombeni msaada wenu je hii mechi niichezeshe au nijiweke pembeni?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...