WATU wengi wanafikiri mafanikio ni kitu ambacho kinatokea
tuu kama ajali lakini mafanikio sio ajali wala sio bahati mafanikio ni
mipango dhahiri ambayo inapangwa na mtu anayeyataka na ayenuia kutoka
katika vilindi vya moyoni mwake kwamba anataka kutoka katika sehemu moja
kwenye maisha ambayo inakuwa ni duni na kwenda sehemu nyingine ambayo
ni ya hadhi nzuri.
Wengi wamekuwa wakijidanganya kwamba ipo siku moja
watafanikiwa (watatoboa)lakini hawana mpango wowote wa kuwawezesha
kufanikiwa katika iyo siku moja na nataka niwaambie kwamba iyo siku moja
haitakaa itokee kama hauna mpango dhahiri wa kupata unachokitaka katika
maisha yako.
Unatakiwa kuwa na picha halisi ya kitu unachokitaka kwanza
ndipo uende ukakitafute, kumbuka kumiliki kunaanzia kwenye akili kwanza
acha kusema nahitaji nyumba nzuri,gari zuri,biashara nzuri, wakati
hujapata picha halisi katika akili yako kile unachokihitaji unataka
kiweje. Vijana wengi wamekuwa wakimaliza chuo Kikuu na kusema nipo
tayari kufanya chochote huu ni ujinga na kutokuwa na maono hivi kweli
kama upo tayari kufanya chochote nkikuambia ukachimbe vyoo utachimba? Be
definate (unataka nini kwanza) na hicho unachokitaka hakikisha una
picha yake kwenye akili yako jinsi kitakavyokuwa ndipo unaanza jitihada
zote zitakazokupelekea kupata kile unachohitaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...