Pichani
kati ni Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli akiwa sambamba na
Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde kwa pamoja
wakiwapungia wananchi wa Mtera (hawapo pichani),ndani ya mji wa Mvumi wilayani Chamwino mkoani Dodoma
Wakazi
wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino wakishangilia jambo
wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za
kuomba kura za Urais jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika
mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dododma.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia Wakazi wa jimbo la Mtera huku akiwamwagia sera
zake za kuomba kura za kuwania nafasi ya Urais katika awamu ya kipindi cha tano,mapema jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dododma.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibakwe,Wilayani Mpwapwa,Ndugu Dkt.Simba Chawene akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa kijiji cha Chipogolo (hawapo pichani),wakati akitokea Iringa vijijini akielekea mkoani Dododma kuanza kampeni zake mkoani humo,kulia kwake ni Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwatazama wananchi waliokuwa wakimuuunga mkono kuwa watampa kura za ndio
Dkt Magufuli akiwapungia Wananchi wa kijiji cha Chipogolo Wilayani Mpwapwa,mara baada ya kuwahutubia mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni,shoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma,Alhaji Adam Kimbisa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Kada mkongwe wa chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.John Samuel Malecela akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni.
Wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino wakishangilia
jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera
zake za kuomba kura za Urais jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dododma.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Isimani Ndugu William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa
Kijiji cha Idodi na Pawaga kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
uliofanyika mjini humo mapema leo asubuhi mkoani Iringa wakati wa
kumnadi Mgombea wa nafasi ya Urais
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli
wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM
Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mapema leo asubuhi
kwenye mkutano wa hadhara wa
kampeni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...