Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Victoria Mwakasege, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 30, 2015 kwa ajili ya kumuaga rasmi akienda kuanza kazi nchini Malawi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya, Judith Sergentine (kushoto) na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya Tanzania, Filiberto Cebregondi, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuwasili nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Victoria Mwakasege, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Sept 30, 2015 alipofika kumuaga rasmi akienda kuanza kazi nchini Malawi. Picha na OMR
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...