Na
Ally Daud –Maelezo
Dar es
salaam
MWILI
wa marehemu wa aliyekuwa Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi
wa Umma Mhe. Celina Ompeshi Kombani (56) umeagwa leo Katika Viwanja vya
Karemjee jijini Dar es salaam.
Waziri huyo ambae pia alikuwa mgombea ubunge Jimbo
la Ulanga Mashariki amefariki dunia Septemba 24, mwaka huu katika hospitali ya
Apollo Nchini India kutokana na ugonjwa wa saratani ya kongosho.
Maelfu
ya waombolezaji yakiongozwa na Makamu wa
Rais wa Tanzania Dkt. Galib Bilal pamoja na Mke wa Baba wa Taifa Mama Maria
Nyerere na Mke wa Rais wa Tanzania Mama Salma Kikwete katika hafla fupi ya
kuaga mwili wa marehemu kabla ya kusafirisha kuelekea Morogoro kwa ajili ya
mazishi .
Wawakilishi
wa mashirika na viongozi mbalimbali wa nchi walihudhuria katika viwanja hivyo
wakiwemo mawaziri wa Tanzania Bara na Visiwani wakiongozwa na Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda ili kutoa heshima za mwisho
kwa marehemu.
Marehemu
Kombani anatarajiwa kuzikwa kesho katika shamba lake huko Morogoro baada ya
waombolezaji kupata nafasi ya kutoa heshima za mwisho katika viwanja wa Jamhuri
mjini humo.
Aidha
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda ametoa pole
kwa wafiwa na kusisitiza kwamba jamii iendeleze ya yaliyoachwa na marehemu kwa ajili ya
kujenga Taifa letu kwani alikuwa mstari wa mbele katika kupigania kuondoa
malipo hewa ya watumishi wa Umma, kufanyakazi kwa bidii na kujawali watu .
Mbali
na hayo Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema wamepokea taarifa hizo
kwa mstuko mkubwa kwani hawakutarajia kuachiwa pengo na Celina Kombani.
Vile
vile Mwenyekiti na mwakilishi wa kituo cha kulelea yatima Good Hope Family ya Kigamboni
Bw. Omari Rajabu amewaasa viongozi waliobakia kutowasahau kwani wamepoteza mama
yao wa dunia ambaye alikuwa mstari wa mbele kuwapigania watu wasiojiweza.
Marehemu
Kombani ameacha mume , watoto watano na wajukuu wanne pia ameacha pengo kubwa
katika Serikali ya Jamhuri wa Muungano Wa Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mama Maria Nyerere, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kushiriki kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
Spika wa Bunge la Jamhuri, Mama Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
Picha na OMR
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...