Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka kukagua
moja kati ya Visima vinne vya Maji safi na salama wakati alipofika
katika Kijiji cha Kigunda Wilaya ya Kaskazini A Unguja kwa ajili ya kukagua
mradi huo wa maji, leo Sept 10, 2015. Mradi huo unaosimamiwa na Kijiji hicho
umegharamiwa na Mhe. Makamu wa Rais kutokana na maombi ya wananchi hao
waliokosa maji kwa miaka mingi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kigunda,
baada ya kukagua mradi wa Maji safi na salama katika Kijiji cha Kigunda Wilaya
ya Kaskazini A Unguja kwa, leo Sept 10, 2015. Mradi huo unaosimamiwa na Kijiji
hicho umegharamiwa na Mhe. Makamu wa Rais kutokana na maombi ya wananchi hao
waliokosa maji kwa miaka mingi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Msingi wa Msikiti wa Shule ya Msingi Kigunda,
baada ya kukagua mradi wa Maji safi na salama
unaosimamiwa na Kijiji hicho ambao umegharamiwa na Mhe. Makamu wa Rais
kutokana na maombi ya wananchi hao waliokosa maji kwa miaka mingi. Kulia kwake
ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Makame Madina.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha
Bwereu, Juma Nyange Omari, wakati alipofika kukagua moja kati ya Visima vinne
vya Maji safi na salama wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi huo katika
Vijiji vya Kigunda na Bwereu Wilaya ya Kaskazini A Unguja, leo Sept 10, 2015.
Mradi huo unaosimamiwa na Kijiji hicho umegharamiwa na Mhe. Makamu wa Rais kutokana
na maombi ya wananchi hao waliokosa maji kwa miaka mingi. Picha na OMR
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...