Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akishiriki kwenye ibada ya kumwombea Marehemu Hulda Kibacha, Mdhamini na Mjumbe wa Bodi ya WAMA iliyofanyika nyumbani kwa marehemu eneo la Ada Estate tarehe 2.9.2015. Aliyekaa kushoto kwa Mama Salma ni Mheshimiwa Zakhia Meghji na kulia ni binti wa marehemu Nampombe Kibacha.
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mdhamini wa Taasisi ya WAMA Mama Hulda Kibacha aliyefariki dunia tarehe 28.8.2015 hapa Dar Es Salaam. Marehemu Kibacha aliwahi kufanya kazi Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).  
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (katikati) kwa kushirikiana na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migiro (kushoto) na Mama Zakhia Meghji (kulia) wakiweka shada la maua kwenye kaburi LA Marehemu Hulda Kibacha aliyezikwa katika makaburi ya Kinondoni tarehe 2.9.2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...