Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akimfariji Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda (kuhosto) ambaye
alifiwa na Mama yake , Hajjat Pili Mlolwa Rehani, nyumbani wa marehemu,
Tanata Magengeni jijini Dar es salaam Septemba 17, 2015. Kuliani Mama
Hasina Kawawa.
Makamu wa
Rais,Dkt. Mohamed Bilal akimfariji mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda
wakati alipokwenda Tabata magengeni jijini Dar es salaam, nyumbani kwa
marehemu, Hajjat Pili Mlolwa Rehani ambaye ni mama wa Mama Tunu,
aliyefariki Septemba 17, 2015. Kulia ni Mama Hasina Kawawa,watatu kulia
ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na
wanne kulia ni Naibu Waziri wake Pindi Chana.
Makamu wa Rais Mohammed
Bilal akishiki kubeba jeneza lenye mwili wa Hajjat Pili Mlolwa
Rehani,mama yake Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda katika sala
ilitofanyika nyumbani kwa marehemu, Tabata Magengeni jijini Dar es salam
Septemba 17,2015.
Inna Lillahi Wainna Ilayhi Rajiun. Poleni sana wafiwa na pole sana Mama Tunu Pinda. Mwenyeez Mungu amjaaliye safari ya salama na amughufirie kwa yote Marehm Bi Hajjat Pili Mlolwa Rehani ampumzishe palipo pema peponi - Ameen. Mwenzetu katangulia nasi sote umauti ndio khatamia yetu, Mola awape faraja na subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa, In Sha Allah.
ReplyDelete