Afisa Masoko wa Airtel kanda ya ziwa akiongea na mawakali mara baada
ya kuendesha seminar inayowapatia fulsa Mawakala wa Airtel Money
nchini nzima kupata mikopo kupitia simu zao za mkononi
Wakala wa Airtel Money katika maeneo ya Metro Mwanza, Bwn John Hainga
akichangia mada wakati wa semina ya mawakala inayowapatia fulsa ya
kupata mikopo isiyo na dhamana ijulikanayo kama Timiza Mikopo kwa
Mawakala
KAMPUNI ya simu za mkononi nchini Tanzania Airtel imeendelea
kuboresha huduma zake kwa wateja hususani wajasiliamali
wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kibiashara, ikiwa ni pamoja
na utoaji wa huduma za Airtel Money , kwa kuwawawezesha mawakala
kupata mikopo inayoitwa " Timiza mikopo kwa Mawakal " Kupitia simu zao
za mikononi.
Airtel imewakutanisha mawakala wa Airtel Money kutoka sehemu
mbalimbali za jiji la Mwanza ili kuwapatia mafunzo ya uboreshaji na
ukuzaji vipato katika biashara zao.
"Ukosefu wa elimu ya uendeshaji biashara kwa wajasiliamali walio
wengi hapa nchini umeendelea kuwa ni tatizo linaloshusha kiwango cha
mapato kwa wajasiliamali kupitia shughuli zao hivyo kuzorotesha uchumi
wa taifa .
Kwa kutambua tatizo hili Airtel imeona ipo haja kuwapatia mafunzo ya
uendeshaji biashara yatakayomwezesha mjasiliamali kutambua njia bora
ya uendeshaji biashara, Ikiwa ni pamoja na utoaji mikopo isiyo na
dhamana kwa zaidi ya mawakala 20,000 kote nchini Ili kusaidia kukuza
biashara za mawakala , kuongeza faida zaidi katika shughuli zao na pia
upatilkanaji wa huduma ya za fedha katika jami". alisema meneja kanda
ya ziwa wa Airtel, Bwana Raphael Daudi.
Kwa upande wake mmoja ya wakala aliyehudhuria semina hiyo bwana John
Paschal alisema" tunayofuraha kuwezesha kupata mikopo kupitia huduma
hii ya Timiza mikopo kwa mawakala. Na hii itaturahisishia kuboresha
biashara zetu kwani sasa tuna uhakika wa mitaji. Lakini pia mafunzo
haya yatatusaidia sana katika kutunza mahesabu na kuendesha biashara
zetu kwa ufanisi zaidi."
Airtel katika kukabiliana na changamoto za kijamii na kiuchumi kwa
wateja wake imefanikiwa kuzindua huduma hii ya timiza mikopo kwa
mawakala, huduma itakayowawezesha mawakala wa airtel money kote
nchini kupata mikopo isiyo na dhamana ya kuanzia sh. 50,000/- hadi
500,000/-
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...