Meneja Ufanisi wa Mgodi wa Dhahabu wa
Bulyanhulu, BGML, unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, Elias Kasikila, (kushoto),
akiagana na baadhi ya vijana wanaokwenda kuhudhuria mafunzo ya ufundi chini ya
mpango wa IMTT unafadhiliwa na mgodi huo, wakati wa hafla ya kuwaaga
iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye eneo la mgodi, huko Msalala mmoani
Shinyanga. Mgodi huo umetuamia kiasi cha zaidi ya nusu bilioni kila mwaka kufadhili mpango huo
Na K-VIS MEDIA
MGODI
wa dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji na
utafutaji madini ya Acacia, umetumia kiasi cha zaidi ya shilingi nusu bilioni
kila mwaka, kufadhili mafunzo ya ufundi kwa vijana, chini ya mpango wa IMTT.
Mpango
wa kufadhili mafunzo ya IMTT, (Integrated Mining Technical Training), ulianzishwa
mnamo mwaka 2009, ambapo mgodi huo hutoa fedha kufadhili elimu hiyo kwa vijana
wenye elimu ya kidato cha nne ambao walisoma kwenye shule zilizoko vijiji 14 vinavyozunguka
mgodi huo na kushindwa kuendelea na kidato cha sita kwa sababu mbalimbali lakini
wawe na umri usioozidi miaka 25.
Akizungumza
kwenye hafla ya kuwaaga vijana 20 kutoka vijiji hivyo kwenye mgodi huo, mwishoni
mwa wiki ambao wameenda kuanza mafunzo hayo yanayochukua muda wa miaka kati ya
mitatu na miwili kwenye chuo cha VETA-Moshi, Menenja Ufanisi (OE),wa BGML,
Elias Kasikila, alisema, ufadhili huo ni utekelezaji wa sera ya mgodi
kushirikiana na wenyeji wao, (wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka mgodi),
katika kujenga mahusiano mema.
Akielezea
utaratibu wa kuwapata vijana hao, Kasikila alisema, waombaji hupeleka maombi
yao kwenye ofisi za serikali za vijijina kisha maombi hayo kukabidhiwa kwa
uongozi wa mgodi ambao huyaachuja kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.
“Sharti
muombaji awe amefaulu masomo ya Kiingereza na Hisabati, lakini kupitia kitengo
chetu cha usalama, vijana hao huchunguzwa tabia zao huko walikotoka, ikiwa ni
pamoja na kufanyiwa vipimo vya kiafya na wanaokidhi vigezo hivyo huchaguliwa.”
Alifafanua
Mafunzo
yanayotolewa ni pamoja na ufundi umeme kwa miaka mitatu, fitting na uchomeleaji
vyuma, kwa miaka miwili, Diesel mechanic and Instrument, kwa miaka mitatu.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...